Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko UWADAR wataka nauli Dar iongozeke kwa Sh 400
Habari Mchanganyiko

UWADAR wataka nauli Dar iongozeke kwa Sh 400

Katibu wa Umoja wa Usafirishaji Abiria Mkoa wa Dar es Dalaam (UWADAR), Selemani Kimomwe,
Spread the love

UMOJA wa Usafirishaji Abiria Mkoa wa Dar es Salaam, umependekeza bei ya nauli ipande kwa Sh. 400, ili kukabiliana na ongezeko la gharama za usafirishaji zilizochangiwa na kupanda kwa bei ya mafuta na kushuka kwa thamani ya Shilingi ya Tanzania dhidi ya Dola ya Marekani. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mapendekezo hayo yametolewa Katibu wa Umoja wa Usafirishaji Abiria Mkoa wa Dar es Dalaam (UWADAR), Selemani Kimomwe, katika kikao cha Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) cha kupokea maoni ya wadau juu ya bei za nauli.

“Kwa maoni yetu UWADAR tunaomba ongezeko la Sh. 400 la nauli kutoka kila nauli, mfano nauli ya Sh. 500 iongezeke kutoka Sh. 500 kuja Sh. 900, kwa ruti tu. Tunaamini maombi yetu yatafanyiwa kazi,” amesema Kimomwe.

Kimomwe amesema gharama za usafirishaji zimeongezeka hali iliyopelekea baadhi ya wamiliki kuondoa magari yao barabarani.

Ametaja baadhi ya gharama hizo ikiwemo ya faini zinazotozwa na mamlaka mbalimbali ikiwemo Jeshi la Polisi, pindi magari yao yanapokuwa chakavu kwa kushindwa kuyatengeneza.

“TANROADS tunalipa faini nyingi sana ambazo hazina msingi ukiangakia Jeshi la Polisi linapambana na sisi. Ukiangalia gharama inafikia kipindi inamuelemea mmilimi na kufanya asiweze kukiendesha,” amesema Kimomwe.

1 Comment

  • Kupanda kwa thamani ya dola inahusu nini dala dala? Kwani wao wanalipa mishahara kwa dola? Acheni uzandiki
    Kama nauli ikipanda mara dufu je na mishahara ya watumiaji wa daladala itapanda?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

NMB yafadhili ziara ya mafunzo machinga, bodaboda Dar nchini Rwanda

Spread the loveBENKI ya NMB imefadhili ziara ya siku nne ya mafunzo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Waliopata Division one St Anne Marie Academy waula, Waahidiwa kupelekwa Ngorongoro, Mikumi

Spread the love WANAFUNZI wa shule ya St Anne Marie Academy waliofanya...

Habari Mchanganyiko

Wadau wataka kasi iongezeke marekebisho sheria za habari

Spread the love  WADAU wa tasnia ya habari wametakiwa kuongeza juhudi katika...

Habari Mchanganyiko

TEF yawatuliza wadau wa habari marekebisho vifungu kandamizi

Spread the love  JUKWAA la Wahariri Tanzania (TEF), limewataka wadau wa habari...

error: Content is protected !!