Friday , 29 March 2024
Home Habari Mchanganyiko LATRA yaanza kupokea maoni nauli za mabasi
Habari Mchanganyiko

LATRA yaanza kupokea maoni nauli za mabasi

Spread the love

MAMLAKA ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), imeanza kupokea maoni ya wadau juu ya nauli za mabasi, ili kutafuta nafuu ya changamoto ya upandaji wa bei za mafuta nchini. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Maoni hayo yameanza kupokelewa katika kikao cha wadau wa usafiri, kilichofanyika leo Jumatano, tarehe 13 Aprili 2022, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji LATRA Gillard Ngewe, amewataka wadau hao kutoa mapendekezo yatakayokuwa na tija kwa pande zote mbili.

“Nadhani leo kazi yetu sisi ni kusikiliza maoni na ninaamini maoni yenu yatajielekeza kueleza hali halisi ya sekta ya usafirishaji na haja ya kuonge,a nauli ili kuboresha sekta yety. Naamini kila mtu atajielekeza kwenye hilo,” amesema Ngewe na kuongeza:

“Tumepata maombi ya mapendekezo wanapendekeza nauli ziwe namna gani, naamini watapewa nafasi ya kuuambia umma mawazo yao. Itakuwa nafasi yetu wadau kutoa maoni kuhusiana na mapendekezo hayo na kuekeza sekta ina hali gani, tuone maamuzi yanaelekea wapi kutokana na mapendekezo yaliyoletwa.”

Mwenyekiti wa kikao hicho, Alhaji Juma Fimbo, amewataka wadau kutoa mapendekezo yatakayowezesha uoatikanaji wa nauli nafuu kwa abiria na msafirishaji.

“Tumejumuika hapa kwa maslahi mtambuka matatu, mosi ni usalama uwe wa mwenye basi au abiria, unachohitaji ni usalama sababu bila usalama kama wewe mwenye basi na abiria utapata hasara. Pili ni unafuu hivyo tuko hapa kuhakikisha tunaibuka na nauli nafuu kwa pande zote mbili,” amesema Alhaji Fimbo na kuongeza:

“Sababu mwenye usafiri atakuwa na nafuu kana atarudisha gharama zske anazoingiza kwenye huduma na msafiri atakywa na nafuu kama gharama atazimudula tatu tunataka huduma endelevu, inayoendelea sio inayopotea baada ya muda mtoa huduma anakata pumzi anaondoka.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA waanza utekelezaji agizo la Samia

Spread the loveMamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam...

Habari MchanganyikoKimataifa

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the loveTUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais wa...

Habari Mchanganyiko

Mtandao watetezi wa haki za mazingira Tanzania waundwa

Spread the loveMTANDAO wa watetezi wa haki za mazingira nchini Tanzania, umeundwa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga kuongoza usambazaji wa mitungi ya gesi 10,000 ya Taifa Gas

Spread the loveNaibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga ameahidi kuongoza kwa ufanisi...

error: Content is protected !!