Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Usain Bolt alaghaiwa zaidi ya TSh 27 Bil.
Kimataifa

Usain Bolt alaghaiwa zaidi ya TSh 27 Bil.

Spread the love

BINGWA wa Olimpiki Usain Bolt analenga kurejesha zaidi ya $12.7m sawa na zaidi ya Tsh 27 Bilioni ambazo wakili wake anasema amepoteza baada ya kulaghaiwa. Yameripoti Mashirka ya Kimataifa … (endelea)

Tume ya Huduma za Kifedha ya Jamaica imeanza uchunguzi dhidi ya kampuni ya uwekezaji, Stocks and Securities Limited (SSL).

Mwanariadha huyo aliyestaafu mwenye umri wa miaka 36 alikuwa na uwekezaji na kampuni ya SSL kwa zaidi ya muongo mmoja.

“Tutaenda mahakamani na suala hilo ikiwa pesa hazitarejeshwa,” wakili Linton Gordon alisema.

“Ni jambo la kutamausha sana, na tunatumai kuwa suala hilo litatatuliwa kwa njia ambayo Bw Bolt atarejesha pesa zake na kuweza kuishi kwa amani.”

Meneja wa Bolt Nugent Walker aliiambia Jamaica Gleaner kwamba bingwa huyo mara nane wa Olimpiki aligundua kwamba kuna “kasoro”.

FSC ilisema “inafahamu ripoti za madai ya ulaghai” na kwamba mchakato wa uangalizi utairuhusu kuona uhamishaji wa fedha na dhamana ndani na nje ya kampuni ya SSL.

“Tume ya Huduma za Kifedha ya Jamaika wakati huo huo itaendelea na uchunguzi wake katika masuala yanayohusiana na SSL,” iliongeza.

Kampuni ya SSL ilisema uchunguzi wake wa ndani unaonyesha kuwa mfanyakazi wa zamani ndiye aliyehusika na madai ya udanganyifu na kuongeza kuwa “imelielekeza suala hilo kwa mamlaka husika za kutekeleza sheria”.

Bolt alistaafu riadha mwaka wa 2017 baada ya kushinda medali 11 za dhahabu za Ubingwa wa Dunia na medali nane za dhahabu za Olimpiki.

Wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Beijing ya 2008, Bolt aliweka rekodi mpya za ulimwengu za mita 100 na 200.

Muda wake wa mita 100 wa sekunde 9.572 unasalia kuwa rekodi ya dunia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!