NCHI ya Urusi, imeingilia kati mgogoro unaoendelea Palestina kwa kufanya mazungumzo na ujumbe wa kundi la wanamgambo wa kiislamu, Hamas, ili kutafuta namna ya kumaliza vita na Israel kwa njia ya amani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Tayari ujumbe wa Hamas, umeshawasili nchini Urusi kwa ajili ya kuzungumza na Serikali ya taifa hilo, ambalo halikitambua kikundi hicho kama cha kigaidi, tofauti na ilivyo kwa mataifa mengine.
Ujumbe huo ulioongozwa na Kiongozi Mkuu wa Hamas, Moussa Abu Marzouk, ulikutana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Mikhail Bogdanov, kwa ajili ya mazungumzo.
Hata hivyo, Israel imeitaka Urusi kusitisha mazungumzo na Hamas, kwa madai kuwa imefanya mauaji ya maelfu ya waisrael wasiokuwa na hatia.
Tayari Shadi Barud, Naibu Mkuu wa kitengo cha kijasusi cha Hamas, aliyedaiwa kuhusika katika mipango ya tukio la uvamizi nchini Israel, lililosababisha mauaji ya amelfu ya watu, ameuawa.
Kwa mujibu wa mtandao wa BBC Swahili, taarifa hizo zimetolewa na Jeshi la Ulinzi la Israel, lililodai kuwa, Barud aliuliwa katika shambulio la anga lililofanywa na ndege za kivita.
Wakati mauaji ya kiongozi huyo wa Hamas aliyesuka uvamizi uliofanyika tarehe 7 Oktoba 2023 na kuzua mapigano yanayoendelea hadi sasa, mazungumzo ya kushawishi kundi hilo liwaache huru mateka wa Israel zaidi ya 220 yanaendelea.
Mtandao wa BBC Swahili umeripoti kuwa, wapatanishi kati ya Hamas na Israel wanaendelea na mzungumzo ya kusitiha mapigano kwa muda ili kuruhusu mateka hao waachwe huru hususan wanawake, watoto na wazee.
Leave a comment