Wednesday , 29 March 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Urusi, Ukraine zabadilishana wafungwa wa kivita
Kimataifa

Urusi, Ukraine zabadilishana wafungwa wa kivita

Spread the love

JUMLA ya wafungwa 179 wa kivita wa Urusi na Ukraine wamerejea nyumbani kufuatia mpango wa kubadilishana wafungwa. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Mshauri mwandamizi katika ofisi ya Rais Ukraine,  Andriy Yermak amesema wanajeshi 116 wa nchi hiyo wameachiliwa huru.

Amesema wafungwa wa kivita walioachiwa wanajumuisha waliokuwa katika mji wa Mariupol wakati wa mzingiro wa miezi kadhaa wa Moscow, pamoja na wapiganaji kutoka mkoa wa Kherson na walenga shabaha waliokamatwa wakati wa mapambano makali yanayoendelea ya kuudhibiti mji wa mashariki wa Bakhmut.

Kwa upande mwingine, Maofisa wa ulinzi wa Urusi nao wametangaza kuwa askari 63 wa Urusi wamerejea nyumbani kutoka Ukraine kufuatia ubadilishanaji huo wa wafungwa.

Kati ya wafungwa hao wamo waliotajwa kuwa kutoka kitengo maalum ambao kuwachiwa kwao kulitokana na mazungumzo ya upatanishi na Umoja wa Falme za Kiarabu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Nyumba ya babu yake Makamu wa Rais wa Marekani yatafutwa Zambia

Spread the love  KAMALA Harris, makamu wa rais wa Marekani, amepanga kutembelea...

Kimataifa

Benki ya Uswizi mbioni kuziwekea vikwazo akaunti za siri za Wachina

Spread the love  WAKATI Serikali na Benki ya Uswizi ikichukua hatua kali...

Kimataifa

Netanyau asitisha mipango yenye utata marekebisho mfumo wa sheria

Spread the love  WAZIRI Mkuu wa nchini Israel, Benjamin Netanyahu amesema atachelewesha...

Kimataifa

Raila ahutubia waandamanaji, mabomu yarindima

Spread the loveMSAFARA wa kiongozi wa Azimio la Umoja-One Kenya, Raila Odinga...

error: Content is protected !!