Tuesday , 23 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari
Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the love

MBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na wananchi wa kata ya Nyamrandirira, mkoani Mara, wamechangia fedha na vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa maabara tatu za masomo ya sayansi katika Shule ya Sekondari Seka. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mara … (endelea).

Michango hiyo imeanza kutolewa jana tarehe 3 Febrauri 2023, kupitia harambee iliyoongozwa na Prof. Muhongo, shuleni hapo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Musoma Vijijini, wanavijiji wameamua ujenzi wa maabara hizo ukamilike ifikapo tarehe 30 Juni 2023.

Taarifa hiyo imechanganua ahadi na michango iliyotolewa, ambapo wananchi wameahidi kuchangia 15,000 kwa kila kaya, wakati Diwani wa Kata ya Nyamrandirira,Mwalimu Nyeoje akichangia Sh. 100,000, huku mbunge akihangia saruji mifuko 150, vitabu vya maktaba makasha saba na mahindi gunia nne kwa ajili ya chakula cha wanafunzi.

Katika hatua nyingine, wanakijiji na Prof. Muhongo wamepanga kununua kompyuta na mashine za utoaji nakala, ifikapo tarehe 30 Aprili 2023.

“Wanavijiji wa Kata ya Nyamrandirira na Viongozi wao mbalimbali wanatoa shukrani za kipekee kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa mchango mkubwa, wa ujenzi wa Sekondari yao, unaotolewa wa Serikali anayoingoza ,” imesema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imesema kuwa, Shule ya Sekondari Seka yenye wanafunzi 344 kuanzia kidato cha kwanza hadi tatu na walimu tisa, inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa maabara za masomo ya sayansi ya fizikia, kemia na bailojia, maktaba, jengo la utawala na choo chenye matundu saba. Shule hiyo ilianza rasmi tarehe 5 Julai 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aridhishwa utendaji mabalozi, awapa neno

Spread the loveRais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amewapongeza mabalozi  wanaowakilisha ...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!