Tuesday , 27 February 2024
Home Kitengo Maisha Afya Ukosefu wa huduma za afya wazua taharuki Kilosa
Afya

Ukosefu wa huduma za afya wazua taharuki Kilosa

Spread the love

UKOSEFU wa Zahanati na ubovu wa miundombinu katika kata ya Mabula wilayani Kilosa mkoani Morogoro imesababisha wanawake watatu kupoteza maisha wakati wakiwahishwa kujifungua katika hospitali ya Berega wilayani humo katika kipindi cha mwaka 2015/16, anaandika Christina Haule.

Wakizungumzia changamoto hizo wanawake hao akiwemo Wema Matowe mkazi wa kijiji cha Magera kata ya Mabula amesema kituo cha afya kilichopo katika eneo hilo hakina uwezo wa kuwasaidia kinamama kujifungua kwa upasuaji.

Amesema ukosefu wa huduma za upasuaji umesababisha vifo hivyo katika kipindi cha mwaka 2015/16 na kwamba hali hiyo inaendelea kuwatia wasiwasi wanawake wa kijiji hicho na kata nzima.

Pia amesema ukosefu huo wa huduma za upasuaji husababisha pia wanawake kupata fistula kufuatia kupata uchungu wa muda mrefu hadi wanafikishwa hospitali ya Berega kwa upasuaji.

“Nimeshuhudia kwa macho yangu kinamama watatu wakifa miaka hii ya hivi karibuni, tunapata wasiwasi,,, lakini hali ya uchumi kwetu ndiyo tatizo, tunaweza kukusanya matofali na kujenga zahanati, lakini hatuwezi kukamilisha ujenzi” amesema Matowe.

Naye Hadija Bakari aliiomba serikali ya wilaya kuangalia namna ya kuboresha huduma za kinamama wajawazito katika zahanati ya kijiji hicho kwani huduma zilizopo katika zahanati ya kata ya mabula hazikidhi mahitaji kufuatia kuwa na kipimo kimoja tu cha kuangalia upungufu wa kinga mwilini.

“Yaani ukifika utapimwa tu mimba na UKIMWI lakini hakuna huduma ya kipimo cha wingi wa damu, makundi ya damu na shinikizo la damu magonjwa ambayo humpata au huhisiwa kumpata mjamzito mara nyingi na mtu kutakiwa kwenda hospitali ya Berega ambako ni mbali” amesema

Akizungumzia hilo Diwani wa kata ya Mabula Meshack Chalo alikiri kutokea kwa vifo hivyo katika kata hiyo na kwamba changamoto ya barabara imesababisha kwa kiasi kikubwa wajawazito kupoteza maisha kufuatia kulazimika kupita njia ndefu ya urefu wa km 25 badala ya km 7 ambayo ina eneo korofi la daraja ambalo linatakiwa kujengwa ili kupitika kwa urahisi na kufika hospitali ya Berega pale inapohitajika.

Diwani Chalo alisema, wamekuwa wakiikumbusha Serikali mara kwa mara juu ya ujenzi wa madaraja makubwa matatu yaliyopo kwenye kata hiyo yanayokwamisha shughuli nyingi za maendeleo Zaidi ya kusababisha vifo vya kinamama na watoto wachanga.

Hivyo aliiomba Serikali kusaidia ujenzi wa angalau daraja moja ili kuweza kupunguza tatizo hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Dk. Biteko aagiza uboreshaji huduma za afya kwa wazee

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaTangulizi

Wanawake walalamikia ukubwa kondomu za kike, waomba zipunguzwe

Spread the loveWataalamu wa afya wilayani Ileje mkoani Songwe wameagizwa kuanza kutoa...

AfyaHabari Mchanganyiko

Madaktari wazawa watenganisha watoto mapacha walioungana

Spread the loveHospitali ya Taifa Muhimbili kwa mara nyingine imeandika historia kwa...

Afya

DC Mpanda aagiza maji ya visima yapimwe kudhibiti kipindupindu

Spread the loveMkuu wa Wilaya ya Mpanda, Jamila Yusuf ameziagiza mamlaka za...

error: Content is protected !!