Friday , 19 April 2024
Home Kitengo Michezo Riadha yazidi kuing’arisha Tanzania
Michezo

Riadha yazidi kuing’arisha Tanzania

Wanafunzi wa shule za sekondari Tanzania walipokuwa kwenye mashindano ya Afrika Mashariki
Spread the love

MCHEZO wa riadha umeendelea kuing’arisha Tanzania baada ya kuzoa medali 10 katika michezo ya Afrika Mashariki kwa wanafunzi wa shule za sekondari, yaliyofanyika mjini Moshi, mkoa wa Kilimanjaro, anaandika Jovina Patrick.

Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha michezo mbalimbali kwa wanafunzi kutoka katika nchi za Afrika Mashariki, lakini mchezo wa riadha ndiyo uliofanyikiwa kuibuka kidedea baada ya wanariadha wake kuvuna medali hizo.

Wanafunzi waliofanya vizuri katika riadha na medali walizopata ni Winifrida Makenji ambaye ameshinda medali nne, Jane Maliga ameshinda medali mbili, Mary Emily medali mbili, Catherine Simon medali moja na Sara Joel medali moja.

Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo, akiwapokea wanamichezo hayo amewapongeza na kukili kuwa wameiwakilisha vyema Tanzania na wameitendea haki bedera ya taifa.

Mwakyembe amewaasa wanafunzi hao kuendelea na michezo hiyo na kufanya mazoezi ili siku za baadaye wawe washiriki mashindano makubwa ya Dunia na kuitangaza zaidi Tanzania.

“Kesho na keshokutwa tutapata wawakilishi wazuri katika mashindano ya dunia kama Olimpiki,” anasema Mwakyembe.

Mbali na pongezi Mwakyembe amewataka wanamichezo wote kutoamini ushirikina katika kupata ushindi bali kufanya bidii na mazoezi mazuri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga pesa na mechi za EUROPA leo hii

Spread the love Hatimaye Alhamisi ya EUROPA imefika ambapo leo hii mechi...

Michezo

Leo ni leo nani kutinga nusu fainali UEFA?

Spread the love HATIMAYE Jumanne ya UEFA imefika ambapo leo hii michezo...

Michezo

Anza Jumatatu yako na Meridianbet

Spread the love  IKIWA ni siku nyingine mpya kabisa ya Jumatatu baadhi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC, Yanga wazindua kadi  za kimataifa za uanachama

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kushirikiana na Klabu...

error: Content is protected !!