November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Sh. bilioni 1.5 zanufaisha wakulima

Matrekta ya kilimo

Spread the love

TAASISI ya kifedha ya inayohusika na kukopesha mashine mbalimbali ikiwemo matrekta (EFTA), imeahidi kuendelea kuboresha huduma hizo ili kuongeza nguvu za kukuza uchumi wa viwanda nchini, anandika Christina Haule.

Meneja wa taasisi ya EFTA, Martin Jeremia amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa ambapo amesema tangu wameanza kutoa huduma mwaka 2016 hadi sasa wameshatoa mikopo yenye thamani ya Sh. bilioni 1.5 kwa wakopaji 30.

Jeremia amesema kuwa hadi sasa wametoa mikopo kwa wakopaji mbalimbali wa mashine tofauti ikiwemo matrekta kwa wakulima hao 30 kutoka mkoa wa Morogoro na Dodoma (Kibaigwa), kwa kuwa wana masharti nafuu na riba ndogo ya mkopo ukilinganisha na watu wengine.

Aidha, amesema mashine zinazokopeshwa zinaanzia kiasi cha Sh. mil 20 hadi 220 na kwamba wanakopesha sekta ya elimu, afya, kilimo na biashara kwa vifaa vya ujasiriamali na kuwataka kulipa riba ya 17% na marejesho ya mkopo katika kipindi cha miaka mitatu.

error: Content is protected !!