Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Ujumbe wa mwisho Rais wa Afghanistan kabla ya kuikimbia Ikulu
Kimataifa

Ujumbe wa mwisho Rais wa Afghanistan kabla ya kuikimbia Ikulu

Rais wa Afghanistan, Ashraf Ghani
Spread the love

 

RAIS wa Afghanistan, Ashraf Ghani ameikimbia nchi yake jana Jumapili tarehe 15 Agosti 2021, baada ya Wanamgambo wa Taliban kuuzingira mji mkuu wa nchi hiyo- Kabul. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mkuu wa Baraza la Maridhiano ya Taifa nchini humo, Abdullah Abdullah pia amethibitisha habari hizo kupitia video na kuongeza kuwa ameondoka Afghanistan na inaaminika amekimbilia taifa jirani la Tajikistan.

Kupitia akaunti yake ya Faceebook, Rais huyo ametoa ujumbe wake wa mwisho kabla ya kuikimbia Ikulu.

Ujumbe huo ulianza hivi; Kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema, Mwenye kurehemu

Wapendwa wananchi! Leo, nimekuja na uamuzi mgumu; Ninapaswa kusimama kukabiliana na wanajeshi wa Taliban ambao walitaka kuingia Ikulu au kuondoka katika nchi yangu pendwa ambayo nilijitolea maisha yangu kuilinda kwa miaka 20 iliyopita.

Kama watu wangeamua kukabiliana na uhalifu na uharibifu wa mji wa Kabul, matokeo yake yangekuwa janga kubwa la kibinadamu katika mji huu wenye wakazi zaidi ya milioni sita.

Taliban wamefanikiwa kuniondoa, wako hapa kushambulia Kabul na watu wake. Ili kuepusha damu kumwagika, nilifikiri ilikuwa bora kutoka nje.

Taliban wameshinda hukumu ya upanga na bunduki na sasa wana jukumu la kulinda heshima ya raia wa nchi, utajiri na kujithamini.

Je! wameshinda kwa uhalali? Kamwe katika historia hakuna nguvu waliyopewa wala uhalali kutoka kwa mtu yeyote. Sasa wanakabiliwa na mtihani mpya wa kihistoria; ama watalinda jina na heshima ya Afghanistan au watatoa kipaumbele maeneo mengine na mitandao yao.

Watu wengi na Aqshar wengi wana hofu na hawaaminiki siku za usoni. Kinachohitajika kwa Taliban ni kuwahakikishia watu wote, mataifa, sekta tofauti, akina dada na wanawake wa Afghanistan kupata uhalali wa kuongoza kutoka katika mioyo ya watu.

Watekelezaji wa mpango huo kwa uwazi na kushirikisha umma. Daima nitaendelea kulitumikia taifa langu kwa wakati wowote kifikra na kuendeleza mpango wa kuliboresha. Mazungumzo mengi zaidi kutoka kwangu yatawajia siku zijazo. Nawatakia maisha marefu Afghanistan.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!