Friday , 3 February 2023
Home Kitengo Michezo NMB yazindua Marathon, mapato kutibu wagonjwa Fistula
Michezo

NMB yazindua Marathon, mapato kutibu wagonjwa Fistula

Spread the love

BENKI ya NMB imezindua mbio ndefu (Marathon) ambazo zitakuwa na kauli mbiu ya ‘Mwendo wa Upendo’ zikiwa na lengo ya kuchangia matibabu kwa wagonjwa wa Fistura kwenye hospitali ya CCBRT. Anaripoti Mintanga Hunda, TUDARCo…(endelea)

Mbio hizo zitafanyika kwa mara ya kwanza Septemba 18, mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo wanatarajia kukusanya zaidi ya shilingi 250 kila mwaka, katika kipindi cha miaka minne.

Hafla ya uzinduzi wa mbio hizo ilifanyika leo Agosti 16, 2021, ambapo pamoja na yote waliingia mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Hospitali ya CCBRT, wenye lengo la kukusanya kiasi cha shilingi bilioni moja katika kipindi cha miaka minne.

Katika utiaji wa saini hiyo, upande wa benki ya NMB uliwakilishwa na Afisa Mtendaji Mkuu Ruth Zaipuna, huku upande wa CCBRT uliwakilishwa na Brenda Msangi ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi hiyo.

Akizungumza wakati wa utiaji saini wa makubaliano na uzinduzi wa mbio hizo, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB Zaipuna, alisema kuna kila dalili za kufikia lengo la makusanyo hayo, hasa kutokana na uungwaji mkono waliopata kutoka Kampuni za Bima za Sanlam na UAP, ambazo zimechangia Sh. Milioni 100 (sawa na Sh. Mil. 50 kila moja).

“Lengo ni kukusanya Sh. Bilioni 1, kiasi ambacho ni sawa na Sh. Mil. 250 kila mwaka. Watanzania wajitokeze kuungana nasi katika mbio hizi, ili kuokoa maisha ya wamama wanaoteseka na maradhi ya Fistula.”

“Tuna mwezi mzima wa kujisajili na naamini tunaweza kufikia lengo kwa ushirikiano huu,” alisema Zaipuna.

Mbio hizo zitakuwa na kategori tatu, kilomita 21 (nusu Marathoni), Kilomita 10 na kilomita 5, na washindi wa kwnza hadi wa 10 watapata medali na fedha taslimu.

Kiasi cha fedha watakachojinyakulia washindi katika mbio hizo ni shilingi 1.4 milioni, huku washindi wa pili wakipata medali na kiasi cha shilingi 1.1 milioni, na washindi wa tatu watapata kiasi cha shilingi 700,000 na medali za shaba.

Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa CCBRT, Brenda Msangi, alisema taasisi yake inajisikia faraja kubwa kufanikisha utilianaji saini wa makubaliano hayo, sambamba na uzinduzi wa NMB Marathon 2021, huku akieleza kuwa mashindano hayo yana maana kubwa kwa maelfu ya kina mama wa Kitanzania.

“CCBRT ni wabobevu wa matibabu ya Fistula nchini, na tafiti zetu za awali zilionesha ukubwa wa tatizo miongoni mwa kinamama, lakini gharama kubwa za matibabu unakwamisha wengi wao kupata tiba za maradhi haya.

“Ndio maana tunachukua nafasi hii kuwapongeza NMB kwa uamuzi wao wa dhati wa kuwabeba wamama wa Kitanzania takribani 60 watakaolipiwa Sh. Mil. 250 kila mwaka katika kipindi cha miaka minne.” Alisema Msangi

Ada za kujisajili kwenye mbio hizo ni shilingi 30,000 kwa kilomita 21 na shilingi 20,000 kwa mbio za kilomita 10 na kilomita 5

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

GGML: Uwanja mpya wa Geita Gold FC kukamilika Mei, 2023

Spread the loveUWANJA wa Magogo unaojengwa na Halmashauri ya Mji wa Geita...

Michezo

Wanafunzi chuo Mwalimu Nyerere wapongezwa kwa ushindi

Spread the love  UONGOZI wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (MNMA)...

Michezo

Arsenal waipopoa Manchester United

Spread the loveKLABU ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu England imewatandika Mashetani Wekundu...

Michezo

Mchezaji Singida apoteza maisha mazoezini

Spread the love  MCHEZAJI na kapteni wa timu ya vijana ya Singida...

error: Content is protected !!