KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA), Anthony Kasore, amesema Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, inaendelea kutekeleza mradi wa ujenzi wa vyuo vya ufundi katika wilaya 25 na vya mikoa vinne, ili kukabiliana na changamoto ya wananchi kushindwa kushiriki kwenye shughuli za uchumi kutokana na kukosa ujuzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tabora…(endelea).
Kasore amesema hayo eo tarehge 17 Oktoba 2023, akizungumzia maendeleo ya ujenzi wa chuo cha VETA Wilaya ya Igunga, mkoani Tabora, unaogharimu kiasi cha Sh. 2.6 bilioni, ambapo kikimalika kitahudumia wanafunzi 900 wa kozi za muda mfupi.
Kasore amesema mradi huo unaoendelea kutekelezwa nchi nzima na kugharimu Sh. 70.9 bilioni, umefikia asilimia 98, huku baadhi ya vyuo vikianza kutoa huduma.
“Mradi huu ulikuwa mahususi kutatua changamoto za shughuli za kiuchumi zinazotokea kwenye wilaya mbalimbali na kuhitaji wananchi kushiriki , lakini wameonekana wanakwama kwa kukosa ujuzi wa kushiriki. Serikali iliona vyema kujenga vyuo hivi na Serikali ilihakikisha vinamalizika na kutoa mafunzo,” amesema Kasore.
Leave a comment