Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Uholanzi yaridhishwa na mazingira ya biashara, demkkrasia na utawa bora nchini
Habari Mchanganyiko

Uholanzi yaridhishwa na mazingira ya biashara, demkkrasia na utawa bora nchini

BalozI wa Uholanzi nchini Tanzania, Wiebe de Boer
Spread the love

 

BALOZI wa Uholanzi nchini Tanzania, Wiebe de Boer ameeleza kuridhishwa na mazingira ya biashara na uwekezaji, demokrasia, haki za binadamu na utawala bora nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Balozi Boer ametoa kauli hiyo jana katika hafla ya kuadhimisha siku maalum ya Mfalme wa Uholanzi iliyofanyika tarehe 25 Aprili 2023 Jijini Dar es Salaam.

Alisema mazingira mazuri ya biashara na uwekezaji nchini umevutia wafanyabiashara wengi kutoka Uholanzi kuja kuwekeza Tanzania.

“Kadhalika tumefurahishwa na kuridhishwa na demokrasia nchini, haki za binadamu na utawala bora pamoja na kufunguliwa kwa majukwaa na mikutano ya kisiasa nchini,” alisema Balozi Boer.

Mbali na kuwekeza katika biashara na uwekezaji pia wafanyabiashara wa Uholanzi wamewekeza pia katika sekta za utalii pamoja na kilimo.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax alieleza dhamira ya Serikali ya Tanzania ya kuendeleza uhusiano wa karibu na ushirikiano uliopo kati ya pande zote mbili.

Dk. Stergomena Tax, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Dk. Tax alisema kuwa Uholanzi imeendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali ikiwamo kilimo, mifugo, uvuvi, elimu, nishati, afya, miundombinu, mawasiliano, utalii, usafiri pamoja na mafuta na gesi.

“Kwa mujibu wa takwimu za Kituo cha Uwekezaji nchini, (TIC) hadi kufikia mwezi Machi, 2023 Kampuni kadhaa za Uholanzi zimewekeza Tanzania kwa kiasi cha (USD milioni 1,079.78), na kutengeneza ajira zaidi ya 15,607 katika sekta za kilimo, ujenzi, nishati, maendeleo ya rasilimali watu, mafuta na gesi, mawasiliano, utalii na usafiri.

“Naomba kutumia fursa hii kuzialika kampuni na wawekezaji kutoka Uholanzi kuwekeza katika fursa zilizopo nchini ikiwa ni pamoja na kuwekeza katika miradi ya kimkakati na yenye maslahi mapana ya pande zote mbili,” alisema Dk. Tax

Amesema Serikali imepata mafanikio makubwa katika kuweka mazingira rafiki na mazuri ya biashara kupitia mageuzi ya kiutawala na kisheria na uwekezaji mkubwa katika maendeleo ya miundombinu.

Pamoja na mambo mengine Dk. Tax aliongeza kuwa juhudi zinazofanywa na Serikali zimepungua gharama za kufanya biashara nchini na kuwezesha ufanisi na uundaji wa huduma rahisi, msingi wa kuchochea shughuli za kiuchumi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!