Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Halmshauri Tunduma yacharuka, yataka vikundi 50 kurejesha bilioni 1.2 za mikopo
Habari Mchanganyiko

Halmshauri Tunduma yacharuka, yataka vikundi 50 kurejesha bilioni 1.2 za mikopo

Spread the love

 

HALMASHAURI ya mji Tunduma, wilayani Momba mkoani Songwe imevitaka vikundi vyote vilivyokopa mikopo ya asilimia 10 kurejesha kwa wakati wakati wakiendelea kusubiri maelekeza ya serikali ambayo imesitisha kwa muda kukopesha fedha hizo. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea).

Akizungumza leo tarehe 26 Aprili 2023 Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Fillimon Magesa amesema mapema Aprili mwaka huu Serikali ilisitisha kukopesha vikundi fedha hizo kutokana na changamoto zilizojitokeza.

Amesema kusitishwa kwa zoezi hilo haimaanishi kuwa vikundi vilivyokopa visirejeshe fedha hizo na vile visitakavyoshindwa kurejesha vitachukuliwa hatua.

Kaimu afisa maendeleo ya jamii Tunduma, Edwad Mbembela amesema katika halmashauri hiyo vikundi vilivyokopa ni vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu walikopeshwa fedha za asilimia 10 za mapato ya ndani.

Amesema jumla ya mikopo iliyotolewa katika mwaka wa fedha 2022/2023 ni Sh bilioni 1.2 ambapo kati yake fedha hizo Sh milioni 685 zimetokana na asilimia 10 ya mapato ya ndani huku Sh milioni 519.3 zilitokana na marejesho ya mikopo.

Amesema jumla ya vikundi vilivyokopeshaa fedha hizi ni 66 ambapo 50 ni kundi la vinana na wanawake wakati 16 ni kundi lawenye ulemavu 16.

Mmoja wa wanavikundi aliyekopa fedha hizo ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe, amesema fedha walizokopa wataendelea kurejesha licha ya baadhi yao kuona sitisho la serikali la kwa kuzitaka halmashauri kutotoa mikopo wanaona ni fursa kwao wakidhani hata marejesho hawarejeshi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!