Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tunduma yatenga bilioni 4 kujenga barabara
Habari za Siasa

Tunduma yatenga bilioni 4 kujenga barabara

Barabara ya kiwango cha rami
Spread the love

 

HALMASHAURI ya mji Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe inatarajia kutumia fedha zake za mapato ya ndani Sh bilioni nne kujenga barabara zenye urefu wa kilomita 29.7 pamoja na madaraja tisa. Anaripoti Ibrahim Yassin, Songwe … (endelea).

Akizungumza leo tarehe 26 Aprili 2023 Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Fillimon Magesa amesema tayari mchakato wa kujenga barabara hizo ulianza tangu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani kwani katika mwaka 2021/ 2022  halmashauri ilitenga bajeti ya bilioni 4.

Amesema kiasi hicha cha fedha kilifanikiwa kujenga barabara za lami kilomita 2.7 na za changarawe kilomita 65 na barabara ndogo kilomita 15.48 na zikajenga tena barabara ndogo kilometa 83.18.

Aidha, halmashauri hiyo katika kipindi cha mwaka 2022/23 walitenga bajeti ya bilioni nne zilizotumika kujenga barabara za lami kilomita 2.95 za changarawe kilomita 32.2 na madaraja tisa huku barabara za udongo zikiwa kilomita 9.4  na barabara za udongo kilomita 44.55.

Aliongeza kuwa katika mwaka wa fedha 2023 /24 walipitishwa tena bajeti ya Sh bilioni nne zitazotumika kujenga barabara za lami kilomita 3.83 za changarawe kilomita 9.44 za udongo kilomita 16.43, madaraja manne na kujengabarabara ndogo kilomita 29.7.

Amesema licha ya kupokea fedha hizo kutoka serikali kuu halmashauri kupitia fedha za mapato ya ndani mwaka 2021/22 ilitumia Sh milioni 135 kufungua barabara za Mpemba-Makaburini.

Amesema mwaka 2022/23 halmashauri ilitumia Sh milioni 500 za mapato ya ndani kutengeneza barabara ya lami 0.71 km, kuzunguka stendi mpya ya Mpemba ambapo mchakato wake umeanza.

Magesa ameongeza kuwa lengo kuu la serikali kupitia halmashauri hiyo ni kuhakikisha mji huo unapitika muda wote kwa kuwa ni lango kuu la nchi wanachama za kusini mwa afrika (SADC).

Amesema zaidi ya asilimia 70 ya mizigo inayovushwa bandari ya Dar es salaam inapita katika mpaka wa Tunduma.

Naye kaimu meneja wa Tarura wa halmashauri hiyo, Jerome Lucas amesema halmashauri ya mji Tunduma inamtandao wa barabara za kilomita 230.5 kati ya hizo za lami ni kilomita 6.226, changarawe kilomita 111.21 ndogo za vumbi kilomita 113.064.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

error: Content is protected !!