Monday , 11 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ufisadi watikisa Bunge, wabunge wataka sheria kuwanyonga wezi
Habari za SiasaTangulizi

Ufisadi watikisa Bunge, wabunge wataka sheria kuwanyonga wezi

Spread the love

KITENDO cha baadhi ya wezi wa fedha za umma kutochukuliwa hatua za kisheria, kimewachefua baadhi ya wabunge ambao wametaka sheria mahususi itungwe itakayoweka adhabu ya kuwanyonga hadi kufa watakaobainika pasina shaka kutenda kosa hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Mjadala huo umeibuliwa na Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara, leo tarehe 3 Novemba 2023, bungeni jijini Dodoma, akichangia taarifa za kamati za bunge kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), kwa mwaka ulioshia Juni 2022.

Kamati zilizowasilisha taarifa yake kuhusu ukaguzi huo wa CAG ni, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma.

“Nchi kama Korea kuna watu wananyongwa kwa makosa kama hayo, sasa napendekeza wale watu ambao imethibitika pasipo shaka kwamba wamekula fedha za watanzania, wote walioiba bila kuwoanea huruma hao watu wanyongwe kwenye nchi hii watoke tubaki na watu wema,” amesema Waitara.

Waitara amekazia “watu wanaoonekana wazembe na wana nafasi kwenye umma wafukuzwe kazi, lazima tuwe na watu waadilifu.”

Wakati anatoa mchango wake huo, Mbunge wa Mbogwe, Nicodemas Maganga, alimkatisha Waitara kwa kutaka kumpa taarifa, ambapo alisema “naomba nimpe taarifa mzungumzaji anayeendelea kuongeza, kwanza viongozi wanaofuatilia mdahalo huu, toka mwaka jana nilisema bila kupitisha sheria ya kunyonga watu wizi hatuwezi kuumaliza.”

“Kwa hiyo naungana naye, sheria ya kunyonga sisi wabunge tuipitishe ili kusudi tumalize biashara hii,” amesema Manganga.

Naye Mbunge Viti Maalum, Anatropia Theonest, aliunga mkono katika mjadala huo akisema “hii ripoti (CAG) uliyonayo hapa unaweza ukaona ni wangapi watanyongwa katika hii nchi.”

Akiendelea kutoa mchango wake baada ya kupokea taarifa hizo, Waitara amedai kuwa, wabunge wanahitaji kupata ripoti juu ya hatua zilizochukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa ubadhirifu wa fedha za umma, ambao umebainishwa katika roipoti za CAG.

“Nimeshuhudia kaguzi hizi zikifanyika, ningependa kupata taarifa mimi na wabunge wenzetu, ukaguzi ukifanyika ukabainisha kuna mtu ni mharifu wa eneo fulani ni hatua gani zinazochukuliwa au tunachukua ripoti tunatunza kabatini?”

“Nataka watuambie baada ya ripoti ya CAG wangapi wamefungwa kwa wizi wa fedha za umma, wangapi wamefukuzwa kazi, wangapi wametapika fedha za watanzania masikini, wangapi wana kesi mahakamani? Hii taarifa hatujapewa tungependa tupewe,” amesema Waitara.

Mbunge huyo wa Tarime Vijijini amedai, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, anafanya kazi kubwa kutafuta fedha kwa ajili ya miradi ya maendeleo, lakini jitihada hizo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu kutokana wezi wa fedha za umma kutodhibitiwa.

Waitara amesema kitendo cha mafisadi kutoadhibiwa, kinaweza kufundisha watoto wadogo kujua kwamba kuiba fedha za umma si kosa.

1 Comment

  • Hii report ina mambo mengi ya watanzania kujifunza,kupata taarifa nini kimechukuliwa hatua& matokeo yake..! Kunyonga sio jibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Biteko: Samia ni muumini wa maridhiano sio kwa kuigiza

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Mpango: Sitakufa bali nitaishi

Spread the loveMAKAMU  wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk....

Habari za SiasaTangulizi

Mbowe: Miaka 62 ya uhuru tujenge upya mioyo yetu

Spread the loveWAKATI Tanganyika ikiadhimisha miaka 62 tangu kupata uhuru, Mwenyekiti wa...

Habari za Siasa

Rais Samia asamehe wafungwa 2,244

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewasamehe wafungwa 2,244, huku akiwabadilishia...

error: Content is protected !!