Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Wabunge waibana serikali matibabu watoto wachanga, watumishi wa afya kikaangoni
Habari za Siasa

Wabunge waibana serikali matibabu watoto wachanga, watumishi wa afya kikaangoni

Spread the love

SERIKALI imeagiza watumishi wa afya kuzingatia maelekezo ya wizara ya afya kwamba watoto wote wachanga wapatiwe matibabu kupitia bima ya afya iliyokatwa na wazazi wao. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Imesema watakaokiuka maagizo hayo watolewe taarifa ili wachukuliwe hatua haraka kukomesha tabia hiyo ya kubughudhi wahitaji wa huduma za afya ambao wamekata bima ya afya.

Kauli hiyo imetolewa bungeni jijini Dodoma leo Ijumaa na Naibu Waziri wa afya, Dk. Godwin Molel wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Martha Gwau aliyehoji iwapo Serikali haioni kuna haja ya watoto wachanga kutumia bima za afya za mama zao.

Akijibu swali hilo, Dk. Molel amekiri kuwepo kwa changamoto kwa wazazi wenye bima wanaojifungua watoto wao kushindwa kupata huduma hasa kwenye vituo vya huduma za afya vya sekta binafsi.

Aidha, amesema wizara ilishatoa maelekezo kwa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuhakikisha watoto wachanga wenye uhitaji wa huduma wanapata huduma za afya bila kikwazo chochote.

“Naomba kutumia fursa hii kuelekeza watendaji wa mfuko wa bima ya afya na vituo vyote vya huduma za afya nchini kuhakikisha watoto na wazazi hawapati shida kwani mama yupo na kadi yake inayoonyesha ushahidi wote kuhusu mtoto husika na ni mtoto wangapi kwenye familia.

“Niwaase wazazi na viongozi wa hospitali husika kukomesha kabisa matukio ya kughushi nyaraka ambayo pia ndio yanapelekea kuwepo kwa usumbufu wakati mwingine,” amesema.

Akiuliza swali la nyonge, Mbunge wa Manyoni Magharibi, Yahaya Massare (CCM) amehoji iwapo muswada wa sheria ya bima ya afya kwa wote uliopitishwa bungeni hivi karibu kama unazingatia mtoto mchanga japo kwa miezi mitatu ili apatiwe huduma.

Akijibu swali hilo, Molel amesema sheria hiyo kuanzia sasa itazingatia watoto watakaozaliwa na wazazi wenye kadi za bima watibiwe.

“Naomba niwaasa wabunge, watanzania na watumishi kwamba ukisikia mtoto amenyimwa huduma ilihali mzazi wake ana bima ya afya, tunaomba tupewe taarifa ili mtumishi huyo achukuliwe hatua haraka,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Tunastawisha ufisadi na kuchukia matunda yake

Spread the loveBUNGE la Jamhuri linaloendelea mjini Dodoma, kwa wiki nzima limetawaliwa...

error: Content is protected !!