Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ufanisi STAMICO waivutia Kenya, watua nchini kujinoa
Habari Mchanganyiko

Ufanisi STAMICO waivutia Kenya, watua nchini kujinoa

Spread the love

UFANISI wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO   pamoja na Wizara ya Madini kwa ujumla umetajwa kuvutia Serikali ya Kenya kuja Tanzania kujifunza utekelezaji wa shughuli  mbalimbali  za uchimbaji madini. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Madini na Uchumi wa Bluu nchini Kenya,  Elijah Mwangi katika ziara yake  ya  wiki moja akiambatana  na ujumbe wa wataalamu sita kutoka nchini humo waliokuja kujifunza na kuona jinsi STAMICO na Wizara ya Madini kwa ujumla wanavyofanya shughuli zake.

Mwangi ameipongeza STAMICO na kusema kuwa imekuwa  ikifanya vizuri katika  kuendeleza  shughuli  za mnyororo  wa thamani wa uchimbaji madini hivyo  wataendelea kujifunza kwa  namna ambavyo  imefanikiwa katika kuendesha shughuli za madini zikiwemo utafiti, uchimbaji, uchakataji na biashara ya madini

Amesema anaamini kuwa kwa sasa Tanzania inanufaika vya kutosha kutokana na rasilimali hizo kupitia sheria na taratibu zilizowekwa.

“Tumejifunza mambo mengi kwa jinsi gani madini yanaweza kubadilisha maisha ya wanajamii na Taifa kwa ujumla.

“Tumekuja hapa ili kuweza kujifunza, kwa sababu sisi bado ni shirika changa ambalo hatuwezi kujilinganisha na STAMICO ambalo limeanza muda mrefu na hatukuona sababu ya kuchagua nchi nyingine kwa ajili ya kujifunza isipokuwa Tanzania, tunashukuru sana kwa kuwa majirani wema na kufungua milango kwaajili yetu,” amesema Mwangi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO, Dk. Venance Mwasse amefurahishwa na ujio wa ujumbe huo ambao umeona ni vyema kujifunza kutoka Tanzania juu ya shughuli za uchimbaji na usimamizi wa rasilimali madini, huku akiamini kuwa ushirikiano huo utasaidia kukuza diplomasia ya uchumi kati ya nchi hizo.

“Tumejadiliana mengi na tumebadilishana uzoefu wa namna ya kuendesha sekta ya madini, nini kinatakiwa kufanyika hasa kwenye maeneo ya masoko,  kuwawezesha wachimbaji wadogo na usafishaji wa madini ili kuhakikisha maslahi katika shughuli yoyote inayohusiana na utafutaji na uchimbaji wa madini inasaidia kuleta mabadiliko kwenye sekta ndogo ya uchimbaji sambamba  sekta zingine

“Taifa lenye rasilimali linatakiwa kushiriki kikamilifu kwenye uvunaji wa rasilimali hizo, wameona sisi tumefanya vizuri kwenye maeneo hayo na wamekuja kujifunza, tumewaelezea namna tunavyonufaika na asilimia kumi na sita za hisa za serikali kwenye migodi, tumeeleza pia namna ambavyo Shirika hili la Taifa linanufaika kutokana na hii Sekta ya Madini,” alisema Dk. Mwasse.

Dk. Mwasse alisema watahakikisha wanawatembeza wageni hao katika maeneo mbalimbali ya Shirika hilo ili wajionee namna ambavyo shirika hilo limekuwa likifanya kazi kwa vitendo, huku akisema kuwa wataweka msingi mzuri wa ushirikiano.

“Geolojia haina mipaka, lakini nchi ndiyo zenye mipaka kinachopatikana huku huenda kinapatikana pia kule Kenya, kwahiyo sisi tuko tayari kushirikiana nao kwenda kule kuwasaidia kugundua na kuweza kuona ni namna gani wanaweza wakasimamia rasilimali hizo ili ziweze kunufaisha watu wao,” alisema.

Ziara hiyo itahusisha mafunzo sambasamba na kutembelea baadhi ya maeneo ya migodi yakiwemo vituo vya mfano vya uchimbaji  mdogo, kiwanda cha kusafisha dhahabu  na Mgodi  wa STAMIGOLD  unaomilikiwa na Serikali.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

error: Content is protected !!