Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Afya Ubakaji watajwa chanzo fistula wasichana wa umri mdogo
Afya

Ubakaji watajwa chanzo fistula wasichana wa umri mdogo

Spread the love

 

TATIZO la ubakaji limetajwa kuwa sababu ya kuongezeka kwa matatizo ya fistula kwa wasichana wenye umri mdogo. Anaripoti Jonas Mushi, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamebainishwa na Rais Samia Suluhu Hassan leo Jumanne tarehe 5 Julai, 2022, akizindua jengo la mama na mtoto katika hospitali ya CCBRT inayolenga kutoa huduma kwa wajawazito wenye ulemavu, wenye historia ya fistula na wenye historia ya matatizo ya uzazi.

“Lakini nilikua nanong’ona na Brenda (Brenda Msangi CEO CCBRT) akaniambia inasikitisha kesi wanazozipokea mtoto wa miaka 11-12 analetwa hapa ana tatizo la fistula na hii inatokanana watoto kubakwa.

“Wale wanaotubakia watoto wanasababisha tatizo hilo, lakini pia kuna vitoto vidogo kabisa miaka minne mitano sita wanapokelewa hapa wana tatizo la fistula,” amesema Rais Samia na kuongeza;

“Kwahiyo ndugu zangu wanajamii ya Tanzania tuone tatizo hili la ubakaji ambalo kwa kiasi kikubwa macho huko kwenye jamii hatulisemi, hatulipeleki kwenye vyombo vya sheria. Niwaombe sana tupunguze idadi hii kwa kuepuka yae yanayoweza kuepukika, ndoa za utoto mimba za utotoni.”

Amesema Tanzania inakadiriwa kuwa na akina mama kati ya 12,000 hadi 19, 000 wanaoishi na tatizo la fistula. “Kwahiyo huduma bora ndiyo msingi wa kuzuia tatizo hili ili kuzuia vifo vitokanavyo na uzazi.”

Samia amesema mpango wa maendeleo ya taifa wa miaka mitano wa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi ni kupunguza vifo kutoka 301 kwa kila vizazi 100,000 hadi vizazi 220 kwa vizazi hai 100,000 ifikapo mwaka 2025/26 na kupunguza vifo vya watoto kutoka 51 kwa kila vizazi hai 1000 hadi 40 kwa kila vizazi hai 1000.

“Kuwepo hospitali hii ni utekelezaji wa mpango huo mkubwa wa afya wa kupunguza vifo vya kina mama na watoto,” amesema Rais Samia.

Amesema pamoja na jitihada za sekta binafsi ikiwemop CCBRT, Serikali haipo nyuma katika jitihada hizo “amesema Waziri hapa majengo ya aina hii ya mama na watoto yanajengwa katika hospitali kadhaa ndani ya Tanzania na kuna miradi inayoendelea kujenga majengo ya mama na mtoto yako kwenye hospitali za rufaa za mikoa ya Mbeya, Njombe, Simiyu, Geita, Songwe Katavi kilimnjaro, Mwanza, Dar es Salaam, Morogoro na Tabora. Tuna miradi yote ambayo lengo ni kuhudumia mama na mtoto.”

Amesema wanafanya hivyo kwa kulenga kufikia lengo la hadi 2025/26 na kupunga vifo hata zaidi ya lengo hilo.

Rais Samia Suluhu Hassan

Ameongeza kuwa Tanzania imefanya vizuri katika vidokezo vinne vya Umoja wa Mataifa vya kupeleka huduma kwenye jamii kama vile kuzingatia idadi ya watu, jografia iliyopo, kina mama wanaojifungulia vituo vya afya, na viwango vya akina mama wanaopata huduma za dharura.

Amesema huduma ya upasuaji imefikia asilimia 10 ndani ya Tanzania na lengo lililowekwa na Umoja wa Mataifa ni kutoka asilimia tano hadi 15. “Kwahiyo tupo katikati tunaisogelea 15.”

Vilevile amesema akina mama wanaojifungulia kwenye vituo wamefikia asilimia 81 ambayo inaashiria idadi kubwa ya watu na eneo kubwa la kijografia wanaoshiriki mpango huo.

Hata hivyo amesema bado Tanzania haifanyi vizuri katika vidokezo viwili vya umoja wa mataifa ikiwepo kutoa huduma za dharura kwa kina mama na watoto wachanga na kupunguza vifo vinavyotokana na uzazi kwa akina mama na watoto wachanga.

“Hii inaonyesha tuna kila sababu ya kuwekeza zaidi katika utoaji huduma kwenye vituo vyetu na ufanisi wa watoaji huduma nao uangaliwe,” amesema.

Amesisitiza mbali na ujenzi wa vituo lakini pia ufanisi wa watoa huduma nao unatakiwa kuangaziwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

AfyaHabari Mchanganyiko

Marekani kuipa Tanzania bilioni 980 kudhibiti VVU, UKIMWI

Spread the loveSERIKALI ya Tanzania inatarajiwa kupewa msaada wa fedha kiasi cha...

error: Content is protected !!