August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Injinia Hersi kuanza na uwanja Yanga

Mhandisi Hersi Said, Mkurugezni wa uwekezaji Gsm

Spread the love

 

Mgombea wa nafasi ya Urais katika klabu ya soka ya Yanga ya Jijini Dar es salaam Injinia Hersi Saidi leo 5 julai, 2022 ametangaza vipaumbele vyake akiwa kama mgombe wa nafasi ya Uraisi huku akiahidi kuanza na mchakato wa ujenzi wa uwanja wa mechi utakaojengwa maeneo ya kaunda_Jangwani . Anaripoti Damas Ndelema Tudarco…… (endelea) 

Uchaguzi wa klabu hiyo, utafanyika Tarehe 9 Julai mwaka huu, ukiwa ni uchaguzi wa kwanza wa klabu ya Yanga toka walipofanya mabadiliko ya katika kwenye mfumo wa uwendeshaji wa klabu hiyo.

Akizungumza katika mkutano huo na waandishi wa habari ikiwa ni siku ya kwanza tangu kufunguliwa kwa kampeni hizo kwa wagombea Hersi amesema kuwa ataanza na miundo mbinu ya klabu kwa kuanza na ujenzi wa uwanja wa mechi wenye uwezo wa kuingiza mashabiki elfu ishirini.

Uwanja huo ambapo kwa mujibu wa ahadi zake utajengwa kwenye eneo la Kaunda, yalipo makao Makuu ya klabu hiyo sambamba na kuboresha jingo la klabu hiyo na kuendelea na kituo cha mazoezi cha Kigamboni.

Pia mgombea huyo alizungumzia juu ya mabadiliko ya muundo wa klabu na kuimarisha uchumi wa klabu kupitia miradi ya usajili wa wanachama na mashabiki , kuvutia wadhamini mbali mbali na wawekezaji.

“Klabu yetu kupitia kwa wanachama walipitisha mfumo wa mabadiliko Nikiwa mmoja wa waumini wa mabadiliko hayo na ahidi kuyasimamia na kuyaendeleza mabadiliko hayo  kwa mujibu wa katiba yetu “ Hersi

Aidha alizungumzia kuhusu kujenga timu imara kwa timu za vijana na soka la wanawake za U-17, U-20 na Yanga princess na kujenga kikosi kipana na imara kitakacho leta mataji na furaha kwa wana Yanga wote kuanzia makombe ya ndani mpaka kimataifa.

Pia mgombe huyo amesema ataongeza ushirikiano baina ya klabu na wanachama na mashabiki wake pamoja na wadau mbalimbali ikiwemo idara za serikali na sekta binafsi bila kusahau waandishi wa habari na watanzania wote kwa ujumla.

error: Content is protected !!