Friday , 3 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ubadhirifu watawala mikopo ya halmashauri, Serikali kuja na kibano
Habari za Siasa

Ubadhirifu watawala mikopo ya halmashauri, Serikali kuja na kibano

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imesema iko mbioni kuanzisha utaratibu wa kutoa vifaa badala ya fedha, katika mikopo inayotolewa na halmashauri, kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha. Anaripoti Jemima Samwel, DMC … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumatatu, tarehe 31 Mei 2021 na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Patrobas Katambi, akimjibu Mbunge Viti Maalum (CCM), Santiel Kirumba, aliyeiomba Serikali iongeze kiwango cha utoaji fedha hizo.

“Lengo la Serikali ni kuwawezesha wananchi kiuchumi ili wanapokopa warudishe, ziwasaidie wengine kufanya biashara zaidi. Tunatarajia hivi karibuni hasa kwenye mwaka huu wa fedha , katika fedha zinazotolewa tuone tija , hasa twende kukopesha vifaa kuliko fedha , ambazo mara nyingi zinatumika vibaya,” amesema Katambi.

Katambi amesema, hadi sasa mabilioni ya fedha yaliyotolewa na halmashauri kwa wakopaji hayajarejeshwa, ambapo katika Ofisi ya Waziri Mkuu, ilitoa Sh. 4.9 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo, lakini kiasi kilichorejeshwa ni Sh. 700 milioni.

“Mpaka sasa katika mifuko ya fedha za halmashauri, ni mabilioni mengi hayajafanyiwa marejesho. Lakini katika Ofisi ya Waziri Mkuu peke yake, tulitoa Sh. 4.9 bilioni. Kati ya fedha hizi, ni Sh. 700 milioni tu, ambazo zimerudishwa. Zaidi ya Sh. 4 bilioni hazijarejeshwa,” amesema Katambi.

Naibu Waziri huyo Ofisi ya Waziri Mkuu, amesema chanzo cha matumizi mabaya ya fedha hizo, ni kusambaratika kwa vikundi vya mikopo, baada ya kupokea fedha hizo, pasina kuzirejesha.

“Tumeona mikopo inayotolewa kwenye halamashuari , vikundi vimekuwa vikijiunga kupata mikopo ile. Baada ya hapo vinasambaratika. Hawaendi kufikia azma ya mikopo hiyo,” amesema Katambi.

Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa, Sura ya 290, iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2018, inaelekeza halmashauri kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani, kwa ajili ya kutoa mikopo kwa makundi hayo.

Katika utoaji mikopo hiyo, wanawake hupata asilimia nne, vijana (4%) na wenye ulemavu (2%)

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaitaka Serikali kuchunguza dawa za asili

Spread the love  KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo...

Habari za Siasa

Kada NCCR-Mageuzi aliyepotea aokotwa porini akiwa taabani, hajitambua

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha NCCR-Mageuzi,...

Habari za Siasa

ACT Wazalendo yataka Jaji Mkuu, Jaji Biswalo wajiuzulu kupisha uchunguzi fedha za Plea Bargaining

Spread the love  CHAMA cha ACT-Wazalendo, kimemtaka Jaji wa Mkuu wa Tanzania,...

Habari za Siasa

Kigogo ACT-Wazalendo: Vyama vya upinzani vilikosea kumpokea Membe, Lowassa

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Ado Shaibu, amesema...

error: Content is protected !!