May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Carlinhos avunja mkataba Yanga, asepa zake

Carlos Stenio Fernandes 'Carlinhos'

Spread the love

 

UONGOZI wa klabu ya Yanga umethibitisha kuvunja mkataba na kiungo wake Raia wa Angola, Carlos Stenio Fernandes ‘Carlinhos’ mara baada ya makubaliano ya pande zote mbili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Carlinhos ambaye alijiunga Yanga kwa mkataba wa miaka miwili kwenye msimu wa 2020/21 akitokea nchini Angola amevunja mkataba huo kutokana na sababu za kifamilia.

Mchezaji huyo aliondoka nchini jana usiku nakurejea kwao Angola mara baada ya kuitumikia Yanga katika kipindi cha msimu mmoja tu.

Taarifa kutoka kwenye uongozi wa klabu ya Yanga ilieleza kuwa makubaliano ya kuvunja mkataba ulifikiwa na pande zote mbili kwa ajili ya manufaa ya klabu mara baada ya mchezaji huyo kuwasilisha ombi la kuondoka.

Katika kipindi cha msimu mmoja aliokaa Yanga Carlinhos hakuitumikia kwa muda mrefu timu hiyo kutokana na kuandamwa na majeruhi ya mara kwa mara.

error: Content is protected !!