
Azza Hilal Hamad
SAA 48 kabla ya Makatibu Tawala wa Mikoa (RAS) kuapishwa, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametengua uteuzi wa Azza Hilal Hamad. Anaripoti Jemima Samwel, DMC … (endelea).
Azza, ambaye aliwahi kuwa mbunge wa viti maalum (CCM), kupitia Mkoa wa Shinyanga, alikuwa miongoni mwa Ma RAS wapya 11 walioteuliwa na Rais Samia, tarehe 29 Mei 2021.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu, tarehe 31 Mei 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa imesema, Azza atapangiwa majukumu mengine.

Kufuatia uamuzi huo, Rais Samia amemteua Prisca Joseph Kayombo kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Simiyu.
Kabla ya uteuzi huo, Kayombo alikuwa Afisa Mkuu wa Utawala na Utumishi katika Wizara ya Fedha na Mipango.
Prisca na wateuliwa wengine wa nafasi hizo, wataapishwa keshokutwa, Jumatano tarehe 2 Juni 2021, Ikulu ya Chamwino Mkoani Dodoma.
More Stories
Askofu Gwajima: Viongozi wa Serikali wanamchonganisha Rais
Rais Samia apandisha viwango vya posho
Msukuma: Mbowe alipa-miss Ikulu