Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Tume haki za Binadamu Pakistan yapinga sheria mpya ya ndoa
Habari Mchanganyiko

Tume haki za Binadamu Pakistan yapinga sheria mpya ya ndoa

Spread the love

TUME ya Haki za Kibinadamu nchini Pakistani (HRCP) imepinga hatua ya serikali nchini humo ya kuingiza tamko la imani ya Kiislam katika fomu ya ndoa inayotamka anayefunga ndoa hiyo ni muislam ilihali kuna dini nyingine nchini humo. Anaripoti Mwandishi wetu … (endelea).

Wanaharakati nchini humo wanadai kuwa mabadiliko ya sheria hiyo ya ndoa ya mwaka 1961 yenye jina la ‘nikahnama’ haikuwa na ulazima kwa kuwa haikuwa na dosari.

“Sheria kama hiyo inapendelea mrengo wa kulia na inaweza kutumika kuchochea vurugu dhidi ya dini kama itatumiwa vibaya”, ilisema ripoti ya HRCP .

Kiongozi mpya aliyechaguliwa, Chaudhry Pervaiz Elahi na serikali yake katika mkoa wa Punjab wa Pakistan tarehe 30 Julai mwaka huu waliidhinisha marekebisho ya Kanuni za Familia ya Waislamu wa Punjab chini ya Sheria ya Familia ya Kiislamu ya 1961, na kutia saini tamko.

Katika taarifa iliyotolewa na serikali ya mkoa, makatibu wote wa mabaraza ya muungano wameagizwa kutumia sheria hiyo ya  nikahnama iliyorekebishwa yenye tamko la kiimani.

Tume hiyo imeeleza kuwa suala la imani ni la mtu binafsi si la kulazimishana hata hivyo Katiba ya Pakistani fungu la 20 imetamka kuhusu uhuru wa imani.

“Madhumuni ya vitendo ya nia nama ni kuthibitisha kwamba pande zote mbili zinafunga ndoa kwa uhuru na kulinda haki ya wanawake ya talaka. Sio kuanzisha imani ya kidini ya mtu binafsi, ambayo ni suala la kibinafsi na linalindwa na Kifungu cha 20 cha katiba,” iliongeza.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari MchanganyikoMakala & Uchambuzi

Kisukari cha mimba ni nini?

Spread the loveKisukari cha mimba ni aina ya kisukari kinachotokea kwa baadhi...

Habari Mchanganyiko

Mafunzo kwa bodaboda 395 yamkuna Meya Dodoma

Spread the loveNAIBU Meya wa Jiji la Dodoma, Asma Karama amepongeza mafunzo...

Habari Mchanganyiko

Samia aagiza huduma za dharura maeneo yaliyoathiriwa na kimbunga Hidaya

Spread the love   RAIS wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania, Samia...

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

error: Content is protected !!