Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko TRC yasitisha kwa muda safari za treni
Habari MchanganyikoTangulizi

TRC yasitisha kwa muda safari za treni

Spread the love

Shirika la Reli Tanzania-TRC limesitisha kwa muda huduma ya safari za treni kutoka Dar es Salaam kuelekea mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, Katavi, Kigoma, Shinyanga na Mwanza kutokana na uharibifu wa miundombinu ya reli. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Taari iliyotolewa jana tarehe 17 Januari 2024 na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano TRC, Jamila Mbarouk imesema shirika limesitisha safari kutokana na uharibifu wa miundombinu ya reli katika maeneo ya Mazimbu, Kilosa na Munisagara mkoani Morogoro.

Pia uharibifu katika maeneo ya Godegode na Guwe mkoani Dodoma, maeneo ya Ruvu junction, Wami, Mvave mkoani Pwani, eneo la Mkalamo Tanga kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Amesema pia shirika hilo limesitisha safari pamoja na mikoa ya Tanga, Kilimanjaro na Arusha.

“Wahandisi kutoka TRC wanaendelea na matengenezo katika maeneo yaliyoathiriwa na mvua zinazoendelea na huduma ya usafiri wa treni zinatarajia kuanza siku ya Jumanne tarehe 23 Januari 2024 katika reli ya kati na kuelekea mikoa ya Kaskazini (Tanga, Kilimanjaro na Arusha linatarajiwa kuanza tarehe 29 Januari 2024 baada ya kukamilika uimarishaji wa miundombinu ya reli.

“TRC inaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza na inawasihi wananchi kuwa wavumilivu katika kipindi cha matengenezo ili kuhakikisha usafiri unarejea katika hali ya usalama,” amesema.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

error: Content is protected !!