Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko TRAMPA yawajengea uwezo watunza kumbukumbu na nyaraka nchini
Habari Mchanganyiko

TRAMPA yawajengea uwezo watunza kumbukumbu na nyaraka nchini

Spread the love

Mwenyekiti wa Chama cha Menejimenti ya Kumbukumbu na Nyaraka Tanzania (TRAMPA) Devotha Mrope amezindua mafunzo maalumu yanayolenga kujenga uwezo wa kitaaluma kwa wataalamu wa taaluma ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Devotha ameyasema hayo juzi Jumatatu katika Mkutano na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema mafunzo haya yanalenga kuwawezesha watumishi wa umma na taasisi binafsi kufanya kazi kwa ufanisi zaidi na uadirifu katika utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka.

“Mafunzo haya yatawakilisha juhudi za TRAMPA katika kujenga uwezo na kuimarisha mifumo ya utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka nchini Tanzania.

” Tunajitahidi kuhakikisha kuwa wataalamu wetu wanapata mafunzo na maarifa yanayohitajika ili kuhakikisha kuwa taarifa na nyaraka zinatunzwa kwa weledi na uadilifu,”  amesema Devota.

Aidha, mafunzo hayo yamepangwa kufanyika Mei 6 hadi 9, 2024 mkoani Iringa katika ukumbi wa Masiti Grand Hall, na yanatarajiwa kuhudhuriwa na wataalamu wa utunzaji wa kumbukumbu na nyaraka kutoka Tanzania bara na visiwani.

Mwenyekiti wa Chama hicho amesema kuwa hii ni fursa kwa washiriki kujifunza mbinu mpya na  bora za utunzaji wa kumbukumbu, uadilifu katika utunzaji wa siri za ofisi, na njia za kisasa za usimamizi wa nyaraka za taasisi.

Pia, kwa kuzingatia thamani ya mafunzo hayo, washiriki watalazimika kulipia gharama ya ushiriki ambayo ni Sh 400,000, ambayo itagharamia uendeshaji wa mafunzo kwa muda wa siku nne.

Sambamba na hilo, Devotha ametoa wito kwa waajiri kuwawezesha watumishi wao kuhudhuria mafunzo haya na kuwalipia stahiki zao.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wanataaluma

kuthibitisha ushiriki wao mapema ili kurahisisha maandalizi ya mafunzo hayo muhimu ambayo yatawezesha kuboresha utendaji na ufanisi katika utunzaji wa taarifa za umma na za binafsi.

“kada hii ni miongoni mwa kada zinazoongozwa na mifumo mingi, sambamba na miongozo kulingana na wakati. Hivyo, inalazimu wataalamu wajengewe uwezo kuendana na mazingira ya wakati husika” amesisitiza Devotha.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

error: Content is protected !!