February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Tigo Fiesta yahairishwa

Spread the love

KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Tigo Fiesta 2018 imesitisha tukio la kilele cha msimu wa tamasha hilo lililopaswa kufanyika leo tarehe 24 Novemba 2018. Anaripori Mwandishi Wetu … (endelea).

Tamasha hilo lilipaswa kufanyika kwenye viwanja vya Leaders vilivyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, lakini kamati hiyo kupitia taarifa yake iliyotoa leo, imesema imesitisha kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake.

“Tunaomba radhi kwa madhara yoyote yatakayosababishwa na hili. Ambao walishanunua tiketi, kwa wale walionunua kupitia Tigo Pesa, fedha zao zitarejeshwa moja kwa moja kwenye simu zao kupitia mtandao, wlaionunua kwenye vituo vya mauzo wafike kwenye vituo wlaivyonunulia tiketi wakiwa na tiketi zao kwa ajili ya kurudishiwa fedha,” inaeleza sehemu ya taarifa hiyo.

Kabla ya kamati hiyo kusitisha tamasha hilo, jana tarehe 23 Novemba 2018 Ofisi ya Afisa Utamaduni Manispaa ya Kinondoni ilitoa tamko la kusitisha kibali cha kufanyika tamasha hilo Leadres Club na kuhamishia katika uwanja wa uwanja wa Tanganyika Peackers ulioko Kawe.

Tamko hilo lilieleza kuwa, usitishaji huo unatokana na malalamiko ya baadhi ya wananchi na wagonjwa waliolazwa hospitalini kutokana na matangazo yanayoambatana na muziki unaopigwa kwa sauti kubwa katika tamasha hilo,na kuhatarisha afya za wagonjwa ikiwemo wa moyo.

error: Content is protected !!