April 17, 2021

Uhuru hauna Mipaka

TFF yaridhia ombi la Yanga, Ninja kuivaa Simba

Spread the love

KAMATI ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Mwenyekiti wake Wakili, Kiomoni Kibamba imeridhia ombi la Yanga kuahirisha kusikiliza shauri dhidi ya mlinzi wa kati wa timu hiyo Abdallah Shaibu ‘Ninja’ katika kikao kilichofanyika Februari 9, 2019. Anaripoti Kelvin Mwaipungu …  (endelea)

Yanga waliomba kamati hiyo ya nidhamu kusogeza mbele shauri la mchezaji wao kutokana kuwa na timu katika mechi za mikoani ya Ligi Kuu hivyo na kuombwa lisikilizwe katika kikao kijacho.

Mchezaji huyo aliitwa mbele ya kamati hiyo wiki moja iliyopita mara baada ya bodi ya ligi kupeleka malalamiko ndani ya TFF kuhusu Ninja kuonesha vitendo visivyo vya uungwana kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union kutoka Tanga.

Ninja alionekana kumpiga kiwiko mchezaji Andrew Simchimba kwenye mchezo uliofanyika tarehe 3, Februari, 2019 kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga na mchezo huo kumalizika kwa sare ya bao 1-1.

Kwa maana hiyo mchezaji huyo anatakiwa kwenda kujitetea au kutuma mwakilishi kwenye kikao kijacho na baadaye kamati hiyo kutoa maamuzi juu ya shauri hilo.

 

 

 

 

 

 

 

error: Content is protected !!