Saturday , 13 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mgogoro wa miaka 40 wapatiwa ufumbuzi
Habari Mchanganyiko

Mgogoro wa miaka 40 wapatiwa ufumbuzi

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula
Spread the love

MGOGORO uliodumu kwa zaidi ya miaka 40 kati ya jeshi la Polisi na Wananchi wa mitaa miwili ya Songambele na Kigoto mkoani Mwanza ambao wanadaiwa kuvamia eneo hilo, sasa umepatiwa ufumbuzi wake. Anaripoti Moses Mseti, Mwanza … (endelea)

Eneo hilo lenye ukubwa wa hekari 41, Wananchi hao wanadaiwa walivamia eneo hilo lenye kaya 461na kujimilikisha eneo lililokuwa mali ya jeshi la Polisi.
Akizingumza katika eneo hilo la Kigoto kwa niaba ya Rais DK. John Magufuli, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumban na Maendeleo ya makazi Angelina Mabula, alisema kuanza sasa ( Jana )wananchi wote wanaoishi eneo hilo ni wakazi halali.
Alisema lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuwatetea wananchi wanyonge, hivyo serikali imeamua wananchi hao kuendelea kuishi eneo hilo.
“Wananchi ambao wanaishi hapa waendelee kama kawaida lakini lile eneo la hekari 17 ambalo halijavamiwa lisiguswe na mtu, pia jeshi la Polisi tutawatafutia eneo lingine.
“Wananchi mnaoishi hapa kuanzia sasa maeneo haya lazima yalasimishwe rasmi ili muweze kuyamiliki kihalali na mpate hati zenu,” alisema Mabula.
Mabula ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ilemela, pia alitaka wananchi hao kulipa  gharama endelea sahahi za umilikishwaji maeneo hayo ambazo zimewekwa na serikali.
Alisema wananchi hao awali walikuwa hawafahamu hatima yao juu ya makazi yao kama yatachukuliwa na jeshi hilo ama vinginevyo, ambapo amedai kuwa hatma ya imepatikana baada ya rais (John Magufuli) kupata taarifa za mgogoro huo na kuchukua aliamua hatua.
Akizungumza baada ya kikao hicho, mmoja wa wananchi hao, Elizabeth Charles alisema maeneo hayo zamani walikuwa wanauziwa na watu na kwamba wait walikuwa hawafahamu kama ni mali ya jeshi la Polisi hivyo waliendelea kuishi eneo hilo kwa muda mrefu.
“Tunamshukuru rais John Magufuli kwa uamuzi wake wa kutusaidia sisi wanyonge kuendelea kuishi eneo hili, sisi hatuna cha kumlipa zaidi ya kumshukru na ukiangalia makosa sio ya kwetu ni ya wale ambao walikuwa wanatuuzia,” alisema Elizabeth.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askofu ataka mafisadi, wauza mihadarati washughulikiwe kumuenzi Sokoine

Spread the love  MHASHAMU Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki Arusha, Isaac...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mafuriko yaua 33 Morogoro, Pwani

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania imetoa tathmini ya athari ya mafuriko...

Habari Mchanganyiko

Wanafunzi 7 wahofiwa kufariki gari la shule likitumbukia korongoni

Spread the love  WANAFUNZI saba wanahofiwa kupoteza maisha, huku watatu wakinusurika katika...

Habari Mchanganyiko

Wazazi, walezi watakiwa kuwa karibu na watoto wao

Spread the love  WAZAZI na walezi wameagizwa kuwalea watoto wao katika maadili...

error: Content is protected !!