Sunday , 5 May 2024
Home Kitengo Biashara Teknolojia ya kidigitali kuleta mapinduzi ya elimu Kusini mwa Jangwa la Sahara   
BiasharaElimu

Teknolojia ya kidigitali kuleta mapinduzi ya elimu Kusini mwa Jangwa la Sahara   

Shameel Joosub, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Group
Spread the love

TEKNOLOJIA za kidigitali na uunganishwaji ni ufunguo wa kuwawezesha vijana wa Afrika kuonyesha uwezo wao. Kwa kuwafungulia milango ya fursa kwa vijana wa Kiafrika kujifunza na kuwaunganisha walimu na wanafunzi ambao wapo maeneo ya mbali na jamii za vijijini, rasilimali hizi zina mchango muhimu kwenye kuboresha mifumo ya elimu ya Kiafrika. Lakini haya yote yatafanikiwa endapo kutakuwepo utaratibu na sera sahihi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).   

Hayo ni miongoni mwa mambo muhimu yaliyoainishwa kwenye ripoti mpya ya utafiti uliofanywa na Vodacom Group, Vodacom, na Safaricom, iliyozinduliwa kwa kushirikiana na taasisi ya Nelson Mandela Foundation. Taarifa ya utafiti, inayojulikana kama “How digital technologies can transform education in sub-Saharan Africa” inaangazia hali ya elimu barani Afrika kwa sasa.

Inaonyesha namna teknolojia za kidigitali na uunganishwaji, zikijumuishwa na mifumo thabiti, kuungwa mkono na serikali pamoja na wadau tofauti katika sekta, zinaweza kutumika kupunguza vikwazo vya elimu barani kote.

Ripoti ya utafiti inaonyeosha kuwepo kwa ongezeko kubwa la upatikanaji wa elimu barani Afrika kati ya miaka 50 mpaka 60 iliyopita, lakini, isipokuwa, kuongezeka kwa upatikanaji wake haimaanishi ukuaji wa ubora wa elimu inayotolewa. Kukiwa na unafuu na uhakika wa uunganishwaji, nyenzo za kidigitali na teknolojia zinatoa suluhisho kwa gharama nafuu na maboresho kukabiliana na changamoto hii, itawawezesha vijana kuunganishwa na wakufunzi wenye ujuzi wa hali ya juu kuwasaidia kuyatumia masomo wanayojifunza kuwa maarifa yenye manufaa kwao.

“Tumeshuhudia hili kupitia miradi na programu zetu za elimu tunazoziendesha, zikilenga upatikanaji wa nyenzo za elimu bora, kuwezesha mtu kujifunza popote alipo, na namna bora ya elimu kwa walimu na wanafunzi kwa sehemu ya jamii za Kiafrika ambazo zina rasilimali pungufu,” alisema Shameel Joosub, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Group.

Programu ya Vodacom ya e-Fahamu ni mfano mzuri, aliongezea Joosub. e-Fahamu ilianzishwa na taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation mwaka 2017 kwa lengo la kuwasaidia walimu na wanafunzi wa shule za sekondari kupata vitabu vya ziada na kiada, maudhui ya elimu pamoja na mitaala iliyopitishwa na Taasisi ya Elimu Tanzania na masomo ya kimataifa bure kwa njia ya mtandao.

Lengo la tovuti hii ni kuunga mkono juhudi za Serikali za kutoa elimu bila malipo kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari nchini. Huduma hii inapatikana kwenye simu za mkononi na kompyuta, bila ya gharama, kwa wateja wote wa Vodacom.

Hii ni sehemu ya mpango wa uunganishwaji wa shule kwa kushirikiana na taasisi ya African Child Projects na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambao unalenga kuzifikia shule 300 za umma nchini kote katika awamu yake hii ya pili. Mpaka sasa wanafunzi takribani 600,000 wananufaika na mpango wa uunganishwaji wa shule nchini kote.

“Upatikanaji wa elimu bora ni muhimu kwenye mapambano dhidi ya umasikini unaoweza kurithishwa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine ikiwemo kuleta usawa. Taasisi ya Nelson Mandela siku zote inasisitiza namna gani elimu ni muhimu, sio kwa kujitambua pekee bali pia kwa kuleta mabadiliko ya mtu binafsi, vilevile kubabidili mwelekeo wa jamii kuwa na usawa, haki, na utu,” alisema Profesa Verne Harris, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa taasisi ya Nelson Mandela Foundation.

Ikiwa hakuna shaka kuwa nyenzo hizi za ubunifu wa kidigitali zina nafasi ya kubadili mfumo wa elimu ya Afrika, bado kuna idadi ya vikwazo kadhaa kwenye upatikanaji wa huduma za kidigitali vinavyozuia vijana wa Kiafrika kuitumia ipasavyo.

Kwa Profesa Jonathan Jansen, mtaalamu wa elimu mashuhuri wa kimataifa na miongoni mwa waandihsi wa ripoti hii ya utafiti anasema, “vikwazo hivi vinahusisha kila kitu kuanzia ukosefu wa nishati ya uhakika ya umeme, msaada wa uhakika wa kiufundi na upungufu wa upatikanaji wa intaneti mpaka vikwazo vya lugha, kutokuwepo kwa utulivu wa kisiasa na vikwazo vya kijamii. Lakini kwa sera sahihi, miundombinu, na utayari katika uwekezaji, maboresho ya kidigitali yanaweza kutoa fursa kwa vijana wa Afrika kufurahia mustakabali wenye usawa, endelevu, na uliounganishwa”.

“Kila kikwazo kinaweza kuondokana kupitia ushirikiano, ushirikishwaji, na mifumo sahihi. Cha muhimu, kutatua vizuizi hivi kunahitaji uhusishwaji wa kisiasa na uungwaji mkono kutoka serikalini ili kuhakikisha mifumo inayowekwa inafaa na inawafikia walimu na wanafunzi wa Kiafrika popote walipo,” aliendelea Profesa Jansen.

Kwa utekelezaji, hii inamaanisha kuendeleza na kutekeleza kanuni ambazo zinaunga mkono elimu ya kidigitali, kujenga ushirikiano wa kimkakati na kuwekeza katika miundombinu ya kidigitali. Kwa kuongezea, serikali za Kiafrika inabidi kuwa wawezeshaji wakuu wa miradi ya ngazi za chini ya elimu ya kidigitali na lazima ziwe na juhudi za pamoja kubadili mafunzo kwa walimu ili kukidhi mahitaji ya kujifunza kidigitali.

Changamoto iliyo mbele yetu ni ngumu, anasema Joosub. “Ni muhimu kujipa muda wa kuelewa mazingira ya uchumi, jamii, na siasa za Afrika ili kuweza kuwaleta kwa pamoja wadau sahihi – kuanzia waliopo ngazi za juu serikalini mpaka wanafunzi waliomo madarasani kutoka kila kona barani – kuja na ufumbuzi.

“Kwa kufanya hivyo, tutaungana kutatua matatizo tunayokabiliana nayo kwa pamoja na kuhakikisha vijana wanakuwa na nyenzo zote wanazozihitaji kuwa na mchango katika jamii zao na kushiriki kikamilifu kwenye uchumi wa kidigitali.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Pata Mil 450 ya Non Stop Drop ukicheza Meridianbet kasino

Spread the love  JIUNGE na promosheni ya Kusisimua iitwayo NON-STOP DROP, inayotolewa...

Biashara

Exim Bank yaendeleza malipo ya kidijitali na Chef’s Pride Dodoma

Spread the love  BENKI ya Exim imeingia makubaliano na Mgahawa wa Chef’s...

Biashara

Cash Days Promo mamilioni yanakusubiri, cheza kupitia Meridianbet kasino 

Spread the love  JIANDAE kwa mshangao wa kustaajabisha Meridianbet kasino ya mtandaoni...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

error: Content is protected !!