Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Makala & Uchambuzi Haya ndio maeneo 12 ambayo Tanzania itafaidika uwekezaji DP World bandarini
Makala & Uchambuzi

Haya ndio maeneo 12 ambayo Tanzania itafaidika uwekezaji DP World bandarini

Spread the love

MJADALA kuhusu makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Dubai ambayo inatarajiwa kuwekeza katika Bandari ya Dar es Salaam umezidi kushika kasi huku wakosoaji wengi wa mkataba huo wakidai hautoi haki kwa Tanzania bali ni wajibu pekee. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea)

Aidha, kutokana na mjadala huo kuzidi kushika kasi, Serikali imeendelea kutoa elimu kwa Watanzania kuhusu mkataba huo uliosainiwa Oktoba mwaka jana na kuidhinishwa na Bunge Juni mwaka huu kwa njia mbalimbali.

Katika mwendelezo wa kutoa elimu hiyo kwa umma, hivi karibuni Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi imetoa takwimu kufafanua faida 12 kubwa ambazo Tanzania inatarajia kuzipata kutoka na uwekezaji wa kampuni ya DP World kwenye bandari ya Dar es Salaam.

Mosi ni kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka masaa 24 tu; Kuongeza idadi ya meli zitakazokuja Bandari ya Dar es Salaam kutoka meli 1,569 zilizohudumiwa mwaka 2021/22 hadi kufikia takriban meli 2,950 ifikapo mwaka 2032/33; Kupunguza muda wa ushushaji wa makontena kutoka wastani wa siku 4.5 mpaka siku 2 na kupunguza muda wa uondoshaji mizigo kutoka masaa 12 mpaka saa 1 tu kutokana na uboreshaji wa mifumo yạ TEHAMA;

Tano ni kupunguza gharama ya usafirishaji wa shehena kutoka nchi za nje kwenda nchi za jirani, kutoka USD 12,000 mpaka kati ya USD 6,000 na USD 7,000 kwa kasha; Kuongezeka kwa shehena inayohudumiwa kutoka tani milioni 18.41 kwa mwaka 2021/22 hadi kufikia tani milioni 47.57 mwaka 2032/33 na kuongezeka kwa mapato ya serikali yatokanayo na kodi ya forodha inayokusanywa katika shehena inayopitishwa bandarini kutoka Shilingi trilioni 7.76 kwa mwaka 2021/22 hadi Shilingi trilioni 26.70 kwa mwaka 2032/33.

Nane ni kuongezeka kwa ajira zinazotokana na shughuli za bandari kutoka 28,990 kwa mwaka 2021/22 hadi 71,907 ifikapo mwaka 2032/33; Maboresho ya magati ya kuhudumia majahazi na abiria ikiwa ni pamoja na kushawishi uingiaji wa meli kubwa za kitali (cruise ships) zitakazo ongeza idadi ya watalii nchini na kuongeza pato la taifa.

Kumi ni kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa TPA katika Bandari zote (knowledge and skills transfer); Uanzishaji wa maeneo huru ya kiuchumi na kuchochea ukuaji wa sekta zingine za kiuchumi zikiwemo: sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi; utali; viwanda na biashara na kuchagiza ukuaji wa sekta ndogo za usafirishaji kwa njia ya reli (SGR, TAZARA na MGR) na barabara; na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Prof Mwafenga ulijiamini katika utendaji wako na degree zako 10 – Maige

Spread the loveKIFO cha Prof Hadley Mpoki Mwafenga- Afisa Usimamizi wa Fedha...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Hii ndio sura halisi ya Rais Samia

Spread the loveKILA zama na kitabu chake. Hizi ni zama za Rais...

Makala & Uchambuzi

Safari ya Siah Malle katika uhandisi inavyoibua vipaji vipya vya wanawake

Spread the loveSiah Malle ni mfano mzuri wa mwanamke ambaye amefanikiwa kuvunja...

Makala & Uchambuzi

Rekodi ya watalii kuandikwa Desemba 2023

Spread the love  WIZARA ya Maliasili na Utalii imesema ifikapo Desemba 2023...

error: Content is protected !!