November 29, 2022

Uhuru hauna Mipaka

TCU wapiga ‘stop’ udahili vyuo vikuu

Katibu Mtendaji TCU, Charles Kihampa

Spread the love

TUME ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imezuia udahili wa wananfunzi wapya katika vyuo vikuu vinne  pamoja na kuamuru wanafunzi wake wa shahada ya kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2018/19 kwenye programu tisa kuhamishiwa katika vyuo vingine. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Katika hatua nyingine, TCU imefuta usajili wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (SMMUCo) na kuamuru wanafunzi wa chuo hicho wanaoendelea na masomo wahamishiwe kwenye kampasi kuu ya SMMUCo iliyopo Masoka wilayani Moshi mkoa wa Kilimanjaro.

Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Charles Kihampa akizungumza na wanahabari leo tarehe 9 Novemba 2018, amevitaja vyuo vinne vilivyozuiliwa udahili ikiwemo Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia (IMTU), Chuo Kikuu Kishiriki cha Askofu Mkuu James (Ajuso), na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Sebastiano Kolowa (SEKOMU).

Prof. Kihampa amesema, chuo cha IMTU kilichopo jijini Dar es Salaam, kimezuiliwa kudahili wanafunzi wa program ya shada ya tiba na upasuaji, shahada ya uuguzi na sayansi, wakati Ajuco cha Songea mkoani Ruvuma kikizuiwa kudahili wanafunzi wa udaktari wa binadamu.

Huku SEKOMU kilichopo wilayani Lushoto mkoa wa Tanga, kikizuiliwa kudahili wanafunzi wa program za shada ya sayansi na elimu, shahada ya sheria na shahada ya elimu na mahitaji maalumu.

error: Content is protected !!