October 2, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba kuivaa Mbabane Swallows Klabu Bingwa Afrika

Patrick Aussems, Kocha Mkuu wa Simba

Spread the love

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba watamenyana dhidi ya Mbabane Swallows katika hatua ya awali ya michuano ya Ligi ya Klabu Bingwa Afrika, inayotarajiwa kuanza mwisho wa mwezi Novemba. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa kati ya tarehe 27-28 mwezi huu katika mzunguko wa kwanza ambao Simba wataanzia nyumbani, huku mchezo wa marudiano ukitarajia kupigwa kati ya tarehe 4-5.

Ikumbukwe Mbabane Swallows ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu ya Swaziland walifanikiwa kuiondosha Azam FC katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika 2017, licha ya sasa kushika nafasi ya nne kwenye msimamo la ligi kuu nchini humo wakiwa na alama 16, baada ya kucheza michezo 8.

Simba watawavaa mabingwa hao baada ya kutoshiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika kwa misimu mitano, toka walivyofanya hivyo mwaka 2012 baada ya kuibuka mabingwa katika msimu wa 2011/12.

error: Content is protected !!