Saturday , 15 June 2024
Home Kitengo Michezo Yanga yaridhia kufanya Uchaguzi
Michezo

Yanga yaridhia kufanya Uchaguzi

Jengo la Yanga
Spread the love

KLABU ya Yanga kupitia kamati ya uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) wameanza zoezi la uchukuaji fomu kwa ajili ya kufanya uchaguzi wa kujaza nafasi zilizo achwa wazi za viongozi wa wawili na wajumbe wanne wa kamati ya utendaji kufuatia kujiuzuru kwao. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).

Uchaguzi huo unatarajia kufanyika 11 Januari, 2019 utakuwa katika nafasi ya Mwenyekiti, Kaimu Mwenyekiti na wajumbe wanne wa kamati ya utendaji ambapo zoezi la uchukuaji fomu limeanza leo katika ofisi za TFF pamoja na klabu ya Yanga huku mwisho wake ukiwa tarehe 13 Novemba, 2018.

Yanga wameamua kuingia katika mchakato huu baada ya kikao kilichofanyika kati yao na uongozi wa shirikisho baada ya kutokea kwa mvutano kufuatia baraza la Michezo Tanzani (BMT) kuwataka klabu hiyo kufanya uchaguzi wa kuziba nafasi hizo huku wakisimamiwa na kamati ya uchaguzi wa TFF.

Akizungumzia mchakato huo Kaimu Mwenyekiti wa Yanga ambaye ameteuliwa na Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo, Thobias Lingalangala hadi hapo uchaguzi wa kujaza nafasi utakapofanyika Januari 13 amesema kuwa uchaguzi utafanyika kama ulivyotangazwa na kamati ya uchaguzi ya TFF.

“Baada ya kikao cha jana kati yetu na TFF ambao ni wasimamizi wetu hakuna tena kikao kingine kilichopangwa kwa sababu tupo kwa ajili ya kutekeleza katiba ya Yanga, taratibu za TFF na FIFA lakini chini ya Serikali yetu hivyo baada ya kikao hicho kinacho fuata ni uchaguzi,” alisema Thobiasi Lingalangala.

Aidha Lingalangala aliongezea kuwa kumekuwa na mambo mengi ya kutaka kuchelewesha uchaguzi kwa baadhi ya wanachama na hivyo kama mtu ana mapenzi na kiongozi yoyote ndani ya Yanga basi amshawishi au amchukulie fomu agombe.

“Kama kuna mtu ana mapenzi na Mwenyekiti Loid Nchunga basi amchukulie fomu agombee, kama kuna mtu ana mapenzi na Francis Kifukwe basi amshawishi amchukulie fomu agombee, kama kuna mtu ana mapenzi na Mwenyekiti Imani Madega basi amshawishi agombee na kama kuna mtu ana mapenzi na Yusuph Manji basi amshawishi na amchukulie fomu agombee”

Gharama za fomu hizo katika nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti itakuwa shilingi 200,000 na wajumbe kamati ya utendaji itakuwa shilingi 100,000.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Serikali yaondoa kodi vifaa vya ‘VAR’

Spread the love  SERIKALI ya Tanzania kupitia Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu...

Michezo

Leo Tanzania ipo dimbani beti na Meridianbet

Spread the love  Mechi nyingi za kufuzu Kombe la Dunia kwa Afrika...

Michezo

Meridianbet inakwambia beti mechi spesho za EURO sasa

Spread the love Wakali wa ubashiri Tanzania Meridianbet wamekuja na Spesho ODDS...

Michezo

Jumamosi ni zamu yako kufurahia mkwanja na Meridianbet

Spread the loveWikendi ndiyo hii imefika jaman na wewe kama mteja wa...

error: Content is protected !!