Monday , 27 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Rais Magufuli aweka tayari magari ya kubebea Korosho
Habari za SiasaTangulizi

Rais Magufuli aweka tayari magari ya kubebea Korosho

Spread the love
RAIS John Magufuli ambaye ni Amiri Jeshi Mkuu, amekagua magari ya Jeshi ya Kikosi ncha Usafirishaji cha 95KJ ambayo yanaweza kutumika kubebea korosho katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Ukaguzi huo umefanyika ili kuwaweka tayari magari hayo, kama wanunuzi wa korosho hawatanunua zao hilo baada ya Jumatatu ya Novemba 12, 2018 jioni.

Rais Magufuli amefanya ukaguzi huo wa magari leo katika kikosi hicho kilichopo Temeke jijini Dar es Salaam, huku akiambatana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo.

Akizungumza na askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wakiwamo madereva wa magari hayo, Rais Magufuli ameagiza kubeba korosho zote zitakazonunuliwa na Serikali iwapo wanunuzi binafsi hawatatii agizo la Serikali ifikapo  Jumatatu saa kumi jioni.

Amesema baada ya kununua korosho, Serikali itatafuta soko na korosho nyingine zitabanguliwa kwa ajili ya soko la ndani na nje ya nchi.

“Nataka kuwahakikishia wakulima wa korosho Serikali ipo na itaendelea kuwapigania, ikifika Jumatatu saa 10:00 jioni, hawa wanunuzi binafsi iwapo hawatajitokeza na kueleza watanunua tani ngapi, Serikali itanunua korosho zote na fedha za kununulia zipo,” amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema Serikali inalazimika kuchukua hatua hizo baada ya wanunuzi binafsi kufanya mgomo licha ya kufanya nao mazungumzo na kufikia makubaliano Oktoba 28, 2018 jijini Dar es Salaam.

“Nimefurahi sana kwamba Jeshi letu la Ulinzi Tanzania lipo tayari kufanya operesheni hii na tunaweza kuiita ‘Operesheni Korosho’, nimeambiwa kuna takriban tani 210,000 za korosho.

“Kule Lindi na Mtwara kuna maghala yanayoweza kuhifadhi tani 77,000 na hapa Dar es Salaam kuna maghala yanayoweza kuhifadhi zaidi ya tani 90,000 na maghala mengine, natarajia kuona zoezi hili linakamilika haraka.

“Kutokana na jambo hili, sasa JWTZ kupitia Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ianze kufikiria kuanzisha kiwanda kikubwa cha kubangua korosho, hata kama itakuwa ni kwa Serikali kutoa fedha za kujenga kiwanda hicho, tuanze kuachana na uuzaji wa korosho ghafi, huo ni utumwa, tuwe na viwanda vyetu na vijana wetu wapate ajira” amesema Rais Magufuli.

Awali, Jenerali Mabeyo amesema JWTZ imetayarisha magari yenye uwezo tofauti 75 ya kubeba jumla ya tani 1,500 kwa mpigo na kwamba, tani nyingine 500 zitabebwa na meli ya kijeshi ambayo inaweza kutia nanga mahali popote katika ufukwe wa bahari.

“Rais na Amiri Jeshi Mkuu tupo tayari kutekeleza jukumu hili,” amesema Mabeyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Wazanzibar watarajia makubwa kutoka NMB Pesa Akaunti

Spread the loveWateja wapya wa Benki ya NMB wa Zanzibar wanatarajia neema...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kinana aungana na Tale kugawa mitungi ya gesi 800

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahman...

Habari za SiasaTangulizi

Makonda amjibu Mwenyekiti UWT, “wananipa nguvu ya kuwapiga spana”

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda amemshukia Mwenyekiti wa...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madeni ya bilioni 219 yalipwa, wadai wengine waitwa

Spread the loveSERIKALI imesema kuanzia Mei mwaka 2021 hadi sasa imelipa madai...

error: Content is protected !!