Tuesday , 26 September 2023
Home Kitengo Biashara Tanzania yapigwa kumbo tuzo ya Chakula Afrika, Kikwete awaibia mbinu…
BiasharaHabari Mchanganyiko

Tanzania yapigwa kumbo tuzo ya Chakula Afrika, Kikwete awaibia mbinu…

Spread the love

RAIS mstaafu Jakaya Kikwete, amezishauri taasisi za utafiti wa kilimo nchini, kuwasilisha tafiti zao kwenye Kamati ya Tuzo ya Chakula Afrika (AFP), ili kushindanishwa na washiriki wengine Afrika. Anaripoti Sulemani Msuya…(endelea).

Kikwete ametoa ushauri huo leo Alhamisi wakati akitangaza mshindi wa tuzo ya mwaka 2023 katika Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC), ambapo Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF), linaendelea.

Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe

Katika tukio hilo Rais Kikwete ameitangaza Taasisi ya Pan Africa Bean Research Alliance (PABRA) ambayo imefanya utafiti wa maharage kuibuka mshindi wa kwanza kati ya washiriki 496.

Amesema AFP imekuwa ikitoa tuzo hizo kwa miaka 18 sasa , hivyo amezishauri taasisi utafiti kutoka Tanzania kushiriki kwa wingi na iwapo zitakidhi vigezo zitaibuka washindi.

Rais Kikwete amesema iwapo tafiti hizo zitajikita kwenye mazao yenye lishe ni rahisi kushinda katika shindano hilo ambalo mshindi anapata dola 100,000 za Marekani sawa na Sh 250 milioni.

Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa AFP,  amesema wamekuwa wakitambua na kusherehekea na taasisi bora ambazo zinaongoza katika mifumo endelevu ya chakula barani Afrika na kwa mwaka huu PABRA ndio imeibuka kidedea

Amesema katika mwaka huu, nchi 47 za Afrika ziliwasilisha kazi 496 ambapo vigezo viliangalia mchango wa mpango katika kupunguza umaskini na usalama wa lishe pamoja na kuboresha maisha kupitia ajira n kazi. 

“Mshindi PABRA amefanya utafiti wa mbegu 650 za maharage ambapo wameonesha aina ya mbegu zinazovumilia ukame, mabadiliko ya tabianchi na nyenye lishe bora kwa mtumiaji,”amesema.

Rais Kikwete amesema mkutano unaoendelea nchini wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Afrika (AGRF-2023), ni fursa nzuri kwa Watanzania kwa kuwa unajadili hali halisi ya kilimo katika nchi za Afrika na kuja na suluhu za kuendeleza sekta hiyo.

Pia, ameeleza kuwa ni sehemu sahihi inayokutanisha wakuu wa nchi wa mataifa mbalimbali, mawaziri, makatibu wakuu, wafanyabiashara wanaojishughulisha na kilimo, wataalamu na watafiti wa kilimo.

“Kuhusu umuhimu wa mkutano imeelezewa sana na mawaziri wetu lakini nasisitizia tu kuwa mkutano huu ni fursa, unakutanisha viongozi wa serikali na wakuu wan chi na wengine muhimu katika sekta hii ya kilimo,” ameeleza.

Amesema AGRF ndio mkutano pekee unaonesha na kujadili jithada za kuleta mageuzi ya kilimo na mifumo ya chakula.

“Unaonesha nchi za Afrika zimefikia hatua gani katika maendeleo ya kilimo, uvumbuzi gani umefanyika katika kilimo lakini pia unakutanisha wawekezaji, wakulima na viongozi wa nchi mbalimbali,” amesema.

“Ukweli ni kwamba Afrika nzima iko hapa. Mkutano huu unafanyika nchini ikiwa ni mara ya pili mara ya kwanza ulifanyika wakati mimi ni Rais mwaka 2012 na Rais AGRA kipindi hicho alikuwa Kofi Annan. Lakini mwaka huu umefanya vizuri zaidi nimeambiwa washiriki ni wengi kiasi cha usajili wa maombi ya kushiriki kuzuiwa. Tayari wamefika washiriki zaidi ya 5,000,” almesema.

Amewataka watanzania kulichukulia jukwaa hilo kama fursa ya kupata wawekezaji, kujifunza zaidi kupitia watalaamu wa kilimo, wanasayansi na watafiti. “Haya ni maonesho ya kilimo katika ngazi kubwa,”

Naye Mjumbe wa Kamati ya AFP, Wanjiru Kamau amesema utafiti uliofanywa na PABRA ukitumiwa na nchi za Afrika  utaenda kumkomboa mkulima.

Amesema wakina mama ndio wakulima wakubwa wa maharage, hivyo ni wazi wakipata mbegu hizo ambazo zimenesha kukabiliana na changamoto kwenye kilimo watapata mazao mengi na kuongeza kipato.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PABRA, Kwani Cloude Rubyogo amesema utafiti huo wamefanya kwa takribani miaka 10 ambapo kila eneo ambalo limeonesha matokeo changa lilikuwa na muda wake usiopungua miaka mitatu hadi minne.

Rubyogo amesema katika utafiti huo nchi 31 zimehusika kwenye utafiti huo ambao umeonesha zaidi ya watu milioni 500 wanatumia maharage.

Mkurugenzi huyo amesema katika utafiti huo aina za mbegu 49 za maharage kutoka Tanzania zimefanyiwa utafiti.

“Nashukuru kwa kupata tuzo hii ya heshima, sio jambo rahisi kwani kwa zaidi ya miaka 10 tunafanya utafiti na leo tumefanikiwa kushinda. Ninachoweza kuahidi ni kuhakikisha tunaendelea na utafiti kwani maharage ni mbegu chakula kizuri sana,”amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

NBC kuchochea ustawi biashara kati ya Tanzania na Afrika kusini.

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza kuhusu dhamira yake...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia apewa tano ujenzi barabara Mtwara

Spread the loveWANANCHI wa Mkoa wa Mtwara, wameishukuru Serikali ya Rais Dk....

Biashara

NMB yazindua hati fungani mpya ya trilioni 1

Spread the loveBENKI ya NMB imezindua rasmi programu mpya yenye hati fungani...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kununua mitambo 15 ya kuchoronga miamba

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Madini imepanga kununua mitambo 15 ya...

error: Content is protected !!