Thursday , 2 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tanzania yaijibu UN kuhusu mradi bomba la mafuta
Habari za Siasa

Tanzania yaijibu UN kuhusu mradi bomba la mafuta

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa
Spread the love


SERIKALI ya Tanzania, imeendelea kusisitiza kuwa, ujenzi wa bomba la mafuta ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), litakalosafirisha nishati hiyo kutoka Hoima nchini Uganda, hadi Tanga, Tanzania, hauna athari kwani unazingatia sheria zote za kimataifa. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 23 Septemba 2022, bungeni jijini Dodoma na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akiahirisha mkutano wa nane wa  Bunge la 12.

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Uganda, inawahakikishia wadau wote ikiwemo Bunge la Umoja wa Ulaya na Jumuiya za Kimataifa, kuwa mradi huu unatekelezwa kwa kuzingatia sheria zote za Tanzania na Kimataifa,” amesema Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa amewahakikisha wadau hususan Umoja wa Ulaya, kwamba ujenzi wa mradi huo unaendeshwa kwa uwazi, pamoja na kuzingatia tahadhari za kimazingira, ulinzi wa mifumo wa kiikolojia sambamba na haki za binadamu.

Amesema, mradi huo utagusa watu 9,513 ikiwemo taasisi mbalimbali, ambapo watu 331 ndiyo watakaohamishwa na kwamba asilimia 85 kati yao wamechagua fidia ya kujengewa makazi ambapo Serikali inajenga nyumba 309 kwa ajili yao.

“Kwa ujumla yote haya yanazingatiwa kwenye mradi huu, hivyo niwatoe hofu wadau wote kuhusiana na utekelezaji wa mradi huu. Serikali ianendelea kutumia njia za kidiplomasia kuhakikisha wadau wanapata taarifa sahihi kuhusu utekelezaji wa mradi huu unaozingatia viwango vyote vya kimataifa,” amesema  Majaliwa.

Waziri Mkuu Majaliwa ametoa kauli hiyo baada ya Bunge la Umoja wa Ulaya, mnamo tarehe 15 Septemba 2022, kupitisha azimio la kulaani ujenzi wa bomba hilo likidai litaharibu viumbe hai na kusababisha mabadiliko ya tabia ya nchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde ataja malengo “Vision 2030”

Spread the loveWAZIRI wa Madini amesema dhana ya “Vision 2030” inakusudia kuiendeleza...

Habari za Siasa

Mavunde aomba bilioni 231.9 bajeti wizara ya madini

Spread the loveWAZIRI wa Madini, Anthony Mavunde leo Jumanne amewasilisha hotuba ya...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu amjibu Fatma Karume kuhusu Rais Samia

Spread the love  MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Slaa: Watanzania iungeni mkono Chadema uchaguzi 2025

Spread the loveMWANASIASA mkongwe nchini Tanzania, Dk. Wilbroad Slaa, amewataka watanzania wakiunge...

error: Content is protected !!