October 6, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Majaliwa aahirisha Bunge, miswada minne na maazimio mawili yapitishwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa

Spread the love

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa, ameahirisha shughuli za Bunge hadi tarehe 1 Novemba 2022,zitakaporejea. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Majaliwa ameahirisha shughuli hizo leo Ijumaa, tarehe 23 Septemba 2022, bungeni jijini Dodoma, katika mkutano wa nane, kikao cha tisa cha Bunge.

Akielezea shughuli zilizofanyika katika mkutano huo wa nane wa Bunge, amesema maswali ya msingi 153 na ya nyongeza 467 ya wabunge, yaliulizwa na kujibiwa na Serikali.

Aidha, Majaliwa amesema katika mkutano huo miswada minne ya sheria ambayo ni Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa wa 2022, Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji wa 2022, Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Fedha wa 2022 na Muswada wa Sheria za Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Namba mbili wa 2022.

Waziri Majaliwa amesema, kupitia mkutano huo wabunge walipitisha maazimio mawili ya Bunge, ambayo ni Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Mktaba wa Nchi Huru za Afrika wa Kuzuia na Kupambana na Ugaidi wa 2004 na Azimio la Bunge la Kuridhia Itifaki ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ya kuongeza mamlaka ya Mahakama ya Afrika Mashariki.

error: Content is protected !!