WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema, hadi kufikia Februari 2022 Serikali imekwisha kulipa malipo ya awali ya ununuzi wa ndege mpya tano. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).
Majaliwa amesema hayo leo Jumatano, tarehe 6 Aprili 2022, wakati akiwasilisha Bajeti ya Ofisi yake kwa mwaka wa fedha 2022/23 Bungeni jijini Dodoma ya Sh.148.89 bilioni na Sh.132.7 bilioni kwa ajili ya Mfuko wa Bunge.
Amesema, Serikali katika mwaka 2021/2022 imeendelea kuliimarisha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ili liweze kutoa huduma bora ya usafiri wa anga ndani na nje ya Tanzania.
Majaliwa amesema, kati ya meli hizotano, ndege moja ni aina ya Boeing 787-8 Dreamliner; ndege mbili aina ya Boeing 737-9; ndege moja aina ya De Havilland Dash 8-Q400; na ndege moja ya mizigo aina ya Boeing 767-300F.
“Kukamilika kwa ununuzi wa ndege hizo, kutaiwezesha Serikali kuwa na jumla ya ndege mpya 16,” amesema Majaliwa
Majaliwa amesema, kutokana na kuendelea kuimarika kwa ATCL, hivi karibuni limefanikiwa kuanza safari katika vituo vya Arusha, Geita, na kurejesha safari za Mtwara na Songea.
Aidha, limerudisha safari za kikanda katika vituo vya Bujumbura, Entebbe, Harare, Lusaka na Hahaya pamoja na kuanzisha vituo vipya vitatu katika miji ya Lubumbashi, Nairobi na Ndola.
Vilevile, Shirika limefanikiwa kurejesha safari ya kimataifa kwenda Mumbai – India pamoja na kuanzisha safari za mizigo kuelekea Guangzhou – China.
Leave a comment