Wednesday , 8 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu Takukuru wambana Mwalimu mkuu, atema bungo
Elimu

Takukuru wambana Mwalimu mkuu, atema bungo

Spread the love

Mwalimu Mkuu wa shule msingi Hanihani, kata ya Igunga wilayani Igunga mkoani Tabora, Joseph Luyega aliyekuwa anatuhumiwa na baadhi wa wazazi wanaosomesha watoto wao shule hapo kwa kuwachangisha fedha Sh. 1000 kila wanapopeleka watoto wao kuandikisha shule, amezirudisha fedha hizo kwa wazazi na kuwaomba radhi. Anaripoti Abdallah Amiri, Tabora … (endelea).

Hatua ya kurudishiwa wazazi fedha zao walizotoa ni baada ya baadhi ya wazazi kwenda ofisi ya tarafa Igunga na ofisi ya TAKUKURU wilaya ya Igunga kumlalamikia mwalimu huyo kwa kuwatoza fedha wazazi kila wanapopeleka watoto wao kuwaandikisha shule chekechea na darasa la kwanza.

Ambapo baada ya wazazi kutoa malalamiko yao katika ofisi hizo mbili, TAKUKURU wilaya ya Igunga ilifika hadi shuleni hapo kisha kumwagiza mwalimu huyo kuwarejeshea wazazi fedha zote walizotoa kwa kuwa hairuhusiwi mzazi yoyote anaepeleka mtoto wake kuandikisha shule kuwatoza fedha.

Hata hivyo, baada ya TAKUKURU kuagiza wazazi warudishiwe fedha zao mwalimu Joseph hakuweza kutekeleza agizo hilo kwa wakati aliopewa na ndipo afisa tarafa Igunga, Simon Marado aliamua kumwagiza mtendaji wa kata hiyo kuitisha mkutano wa wazazi wote wa shule hiyo kwa ajili ya kusikiliza pande zote.

Wakizungumza kwa masikitiko baadhi ya wazazi Ramadhani Abdallah, Dominick Magembe na John Isaya kwenye kikao cha wazazi kilichofanyika kwenye viwanja vya shule hiyo ya msingi Hanihani mbele ya kaimu afisa tarafa Godfrey Steven na afisa elimu kata ya Igunga, Bakari Sarai.

Walisema mwaka jana walikubaliana kuchanga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja ya walimu na kila mzazi anapotoa fedha apewe karatasi iliyogongwa muhuri wa shule hiyo na fedha zipelekwe kwa mhasibu wa kamati ya shule hiyo.

Walisema katika makubaliano hayo pia walikubaliana jengo hilo lijengwe hadi saizi ya boma na baadae likabidhiwe kwa halmashauri ya wilaya Igunga kwa ajili ya kupauwa ambapo jengo hilo lilishafika kiwango hicho hivyo wao hawakupaswa kuchangishwa bila vikao vya wazazi.

Aidha, wazazi hao walishangazwa kuona mwaka 2024 mwalimu akiwatoza fedha wazazi wanaopeleka watoto wao kuwaandikisha shule chekechea na darasa la kwanza na kutowapa wazazi karatasi iliyogongwa muhuri wa shule hiyo huku fedha hizo akikaa nazo nje na maazimio ya wazazi.

Baada ya maelezo ya wazazi, Kaimu afisa tarafa, Godfrey Steven aliwauliza wazazi kuwa mchango uendelee na fedha zisirudishwe kwa wazazi waliotoa au lah, ndipo wazazi waligoma kuendelea kuwachangishwa huku wakitaka fedha zote zirudishwe kwa wazazi waliotoa.

Hata hivyo, wazazi hao walisema wao wako tayari kuchangia maendeleo ya shughuli za shule yao lakini sio kwa kuchangisha wazazi wanaopeleka watoto wao kuwaandikisha shule wakati serikali ilishazuia kuwatoza fedha wazazi wanaopeleka shule watoto wao.

Baada ya wazazi kugoma Steven alimuagiza Mwalimu huyo kurudisha fedha hizo zaidi ya Sh 100,000 na kuomba msamaha jambo ambalo alilitekeleza.

Kwa upande wake mwalimu mkuu huyo, Joseph Kuyega alisema yeye hakujua kama alikuwa amekosea kutoza fedha wazazi kwani alifikiri ni mwendelezo wa michango kwa kuwa shule bado ina mahitaji mengi.

“Nawaombeni mniwie radhi kwa hayo yaliyotokea sikujua kama nimekosea naomba mnisemehe sana wazazi wangu.”

Kwa upande wake afisa elimu kata ya Igunga, Bakari Sarai aliiagiza kamati ya shule kuitisha kikao cha wazazi kwa ajili ya kuzungumza na kutatua changamoto za shule hiyo huku akiwataka wazazi kuendeleza ushirikiano na walimu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari za Siasa

Serikali kuongeza wanufaika mikopo ya elimu ya juu

Spread the loveSERIKALI imesema itaongeza idadi ya wanufaika wa mikopo ya elimu...

ElimuHabari za Siasa

Serikali kufumua mitaala ya vyuo vikuu, ufundi stadi

Spread the loveSERIKALI inakusudia kufanya mapitio katika mitaala na programu za vyuo...

ElimuHabari Mchanganyiko

Chongolo aagiza TAKUKURU kuchunguza ujenzi wa bweni

Spread the loveMkuu wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amemuagiza Kamanda wa...

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

error: Content is protected !!