Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mamia wajitokeza kumuaga Lowassa Karimjee
Habari za SiasaTangulizi

Mamia wajitokeza kumuaga Lowassa Karimjee

Spread the love

MAMIA ya watu wamejitokeza katika Viwanja vya Karimejee jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, huku zoezi hilo likitarajiwa kuongozwa na Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Leo tarehe 13 Februari 2024, mwili wa Lowassa unatarajiwa kuagwa katika Viwanja hivi ambapo viongozi mbalimbali wa kiserikali akiwemo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mawaziri wengine wamehudhuria.

Mbali na mawaziri wa Tanzania Bara, Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa kwanza wa Rais Zanzibar, Othman Masoud Othman na mawaziri kadhaa wa visiwa hivyo, wamehudhuria kwa ajili ya kushiriki shughuli hiyo.

Viongozi wengine wa vyama vya siasa akiwemo Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na viongozi wa dini, wamehudhuria shughuli hiyo.

Jeneza lililobeba mwili wa Lowassa huku likiwa limefunikwa na bendera ya Tanzania, limeingia uwanjani hapo majira ya 10.20.

Shughuli hiyo inatanguliwa na ibada fupi inayoongozwa na Mchungaji Joseph Mlaki, wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Azania Front.

Lowassa anatarajiwa kuzikwa kijijini kwao Monduli jijini Arusha, Jumamosi ijayo ya tarehe 17 Februari mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!