Sunday , 28 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Chadema yaitega CCM kuhusu Lowassa
Habari za SiasaTangulizi

Chadema yaitega CCM kuhusu Lowassa

Spread the love

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeitaka Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kumuenzi Hayati Edward Lowassa, kwa kukamilisha mchakato wa upatikanaji katiba mpya. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 13 Februari 2024 na Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika, katika shughuli ya kuuaga mwili wake wa Lowassa, aliyefariki dunia tarehe 10 Februari 2024.

Mwanasiasa huyo amesema “Lowassa alikuwa na mnyumbuliko wa kisiasa wa kubadilika kutokana na mazingira maana yake aliingia kwenye kura ya maoni ya chama chake kwa muda mfupi akafanya mazingira kujiunga na Chadema ambayo ina miongozo, sera na itikadi tofauti lakini alikubali kujiunga nayo.”

“Wakati wa Bunge Maalum la Katiba tukaunda umoja wa kupigania katiba UKAWA alipokuja alikuta tuna ajenda tofauti na ilani ya uchaguzi tofauti lakini alikubaliana nayo. Yeye alikuja na sera ya elimu akafanya majadiliano akakubaliana na sera yetu.

Awali alikuwa anapinga katiba mpya lakini akafanya majadiliano akakubaliana na hoja ya katiba mpya katika kuleta mabadiliko ndani ya nchi. Wito wangu kwa wadau wote ambao wanamwomboleza Lowassa tukamilishe mchakato wa katiba mpya sababu alikubali na akajiunga na UKAWA,” amesema Mnyika.

Mnyika amesema Serikali inapaswa kubadilisha katiba ili kuruhusu matokeo ya urais kupingwa mahakamani badala ya kutumia maandamano ya wananchi kitendo kinachoweza kuhatarisha usalama na amani.

“Eneo lingine ambalo nimeliona ni baada ya matokeo ya uchaguzi mazingira yalionyesha kuna hujuma kwenye uchaguzi na kulikuwa na njia mbili kukaa kimya na kuingia barabarani kuingiza wananchi barabarani kuishinikiza haki kupatikana, Lowassa akasema kwa taarifa alizonazo vyombo vya dola vimejpanga kumwaga damu hakuna sababu ya kuingia barabarani.

“Hapa naliona funzo ambalo watu wa kwenye mamlaka wajifunze si kila mgombea urais atakuwa na roho kama aliyofanya Lowassa kwamba nguvu ya umma isitumike kudai haki kwa sababu matokeo yake yanaweza kuibua mapambano.

“Ili tusiingie katika hilo mtego wa kutumia nguvu ya umma kupata haki tufanye mabadiliko ya katiba ili mgombea urais matokeo yake yapingwe mahakamani badala ya kwenda barabarani,” amesema Mnyika.

Amesema Lowassa enzi za uhai wake alikuwa anapigania maisha ya wanyonge hususan wa makundi ya chini bodaboda na mamalishe, hivyo ili kumuenzi Serikali inapaswa kutatua changamoto ya ugumu wa maisha inayowakabili wananchi wake.

“Jambo la mwisho nataka kulisemea, ni yake mapito ya Lowassa 2008 wakati wa kujiuzulu kwake kuna mengi ya kujifunza. Mimi rai yangu kwa watanzania wote kama sehemu ya kumuenzi Lowassa na hili jambo nililishughulikia sana kabla ya kuwa mbunge na baada ya kuingia bungeni tukazungumzia masuala ya Dowans, Richmond, mgawo wa umeme na mpaka leo tumekuja kumpa heshima za mwisho kuna mgawo wa umeme katika nchi.

“Lazima kama nchi kama sehemu ya kumuenzi tuhakikshe matatizo ya umeme, mikataba kwenye sekta ya nishati hayarudiwi tena katika taifa letu kwa kuhakikisha tunakuwa na umeme wa kutosha kwa kutumia njia zote za kuzalisha umeme wa kutosha na kuwa na mikataba mizuri,” amesema Mnyika.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mavunde aibana kampuni kutimiza masharti ya mkataba

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameitaka Kampuni ya Xin Tai...

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

error: Content is protected !!