Saturday , 27 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mnyika ataja sababu kumpinga Lowassa Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Mnyika ataja sababu kumpinga Lowassa Chadema

Spread the love

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Mnyika, amesema sababu ya kupinga chama chake kumsimamisha Hayati Edward Lowassa kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, ni kwamba alimtaka awe mwanachama badala ya mgombea. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Mnyika ametoa kauli hiyo leo Jumanne, akizungumza katika shughuli ya kuuaga mwili wa Lowassa, kwenye viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. Lowassa alifariki dunia tarehe 10 Februari mwaka huu akipatiwa matibabu hospitalini.

“Ujio wa Lowassa Chadema kwangu ilikuwa kipindi cha majaribu sana sababu alikuwa na mtazamo tofauti nilitaka aingie kama mwanachama ili aivunie nguvu CCM aongeze mtaji wa kuwa na movement for change tukiunganisha nguvu yetu na ya kwake mgombea yoyote wa Chadema angesimama angepata nguvu lakini wenzangu waliokuwa na mtizamo tofauti aende huyu (Lowassa),” amesema Mnyika.

Mnyika ameeleza” ilikuwa kipindi cha majaribu pengine niliandika kitabu juu ya yali yaliyotokea Kuna mengi mazuri na mengine magumu ambayo yalitokea wakati mchakato wa Lowassa kuingia Chadema na baadae aliporudi CCM.”

Aidha, Mnyika ametaja siri ya Lowassa kuwa na nguvu kisiasa na mtaji mkubwa wa wananchi, akisema ni kutokana na kuanza mapema harakati za kugombea urais ambapo alijenga mtandao mkubwa tangu 1995 alipochuana na rafiki yake wa karibu Jakaya Kiwkete katika kura za maoni CCM.

“Inabidi watanzania wajue kwamba Lowassa alianza kampeni za Urais kabla ya 1995 akiingia kura ya maoni Kwa mara ya kwanza na Kiwkete na baada ya kuteuliwa Mkapa akaendelea na hiyo harakati kulikuwa na mtandao akatengeneza nguvu na Kikwete alipoingia akaendelea hata ilipotokea ajali ya kisiasa tayari alijenga mtandao,” amesema Mnyika.

Amesema Lowassa ni mvumilivu “nilipna uvumilivu pamoja na misukosujo aliyopata ndani ya chama chake kuanzia kujiuzulu, kutoteulwia kwenye kura za maoni kugombea urais lakini ndoto aliendelea kuwa nayo na akiingia Chadema. Watu wajifunze kusimama ndoto zao.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Sauti ya Watanzania waeleza sababu za kuiunga mkono Chadema

Spread the love  KIKUNDI kinachojipambanua katika kupigania rasilimali na uhuru wa nchi,...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jacob, Malisa waachiwa kwa masharti

Spread the love  JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

error: Content is protected !!