Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Elimu St Mary’s yaahidi kuendelea kuwa juu kitaaluma
Elimu

St Mary’s yaahidi kuendelea kuwa juu kitaaluma

Spread the love

CHUO cha Elimu ya Biashara (CBE) kimeahidi kuiunganisha shule ya St Mary’s Mbezi Beach na Maktaba Kuu ya Taifa ili wanafunzi wa shule hiyo wapate fursa ya kusoma vitabu mbalimbali kwa namna rahisi. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Ahadi hiyo ilitolewa mwishoni mwa wiki na Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Kampasi ya Mwanza, Dk Robert Mashenene, wakati akizungumza kwenye mahafali ya 22 ya shule ya sekondari St Mary’s.

Alisema vitabu ni nyenzo muhimu kwa wanafunzi hivyo atafanya jitihada ili ndani ya muda mfupi shule hiyo iwe imeunganishwa na maktaba kuu ya taifa na kuanza kunufaika na vitabu vinavyopatikana ndani ya maktaba zake.

Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Kampasi ya Mwanza, Dk Robert Mashenene, wa pili kulia akiwa kwenye picha na baadhi ya viongozi walipowasili kwenye mahafali ya kidato cha nne ya shule ya sekondari St Mary’s Mbezi Beach wakati wa mahafali hayo mwishoni mwa wiki shuleni hapo.

“Na katika kuwaunganisha kuna gharama huwa zinahitajika nawaahidi kwamba hizo gharama nitatoa mimi kwasababu nataka wanafunzi wetu wanufaike na fursa ya vitabu vinavyopatikana pale,” alisema

Kadhalika, alizitaka shule nchini kuwekeza kwenye Tekmolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na maabara za kisasa ili kulisaidia taifa kupata wataalamu wengi kufanyakazi kwenye sekta ya uhandisi.

“Dunia inakwenda kasi sana kwa hiyo tunavyozidi kuingia kwenye dijitali watahitajika wataalamu wengi sana wa TEHAMA wekezeni katika maabara zenye zana zote za kisasa tuongeze idadi ya wahandisi watakaotumika kwenye miradi mikubwa ya ujenzi,” alisema

Baadhi ya wahitimu wakitoa burudani kwenye mahafali ya kidato cha nne ya shule ya sekondari St Mary’s Mbezi Beach wakati wa mahafali hayo mwishoni mwa wiki shuleni hapo.

“Lazima mjitofautishe na wengine kwa kuwa na maabara za kisasa ambazo zitasaidia kupata wanasayansi wazuri ambao wanahitajika kwenye dunia ya kidijitali,” alisema

Aliwataka walimu na watumishi wote wa shule hiyo washikamane kwani mafanikio waliyopata ni matokeo ya mshikamano na kufanyakazi kama timu moja.

Aliwataka wahitimu wasidhani kuwa kumaliza kidato cha nne ndiyo mwisho wa masomo na badala yake waone kwamba safari ndiyo kwanza imeanza na waendelee kufanya vizuri kwenye masomo.

“Kuna watakaoenda kidato cha tano na wengine vyuoni lakini cha msingi ni nidhamu kokote mtakapokuwa kwasababu nidhamu ni jambo la msingi maishani, nimefarijika sana kuona kuna walimu wanaofundisha maadili na dini,” alisema

Baadhi ya wahitimu wakitoa burudani kwenye mahafali ya kidato cha nne ya shule ya sekondari St Mary’s Mbezi Beach wakati wa mahafali hayo mwishoni mwa wiki shuleni hapo.

Aliwaka wazazi nao kuwahimiza watoto wao kwenda kwenye nyumba za ibada ambako watajengwa kuishi maisha yenye maadili.

Alisema wazazi wanawajibu wa kufuatilia nyendo za watoto kuanzia mavazi na makundi wanayokuwa nayo kwani wanaweza kupoteza mwelekeo wasipodhibitiwa kuwa na mwenendo mwema.

Aliwataka pia watumie simu kufanya mambo ya msingi badala ya kuitumia kwa mambo machafu na yasiyofaa ambayo yamekuwa chanzo cha mmomonyoko wa maadili.

Aliwataka pia kuweka utaratibu wa kuwatafuta wahitimu wa miaka ya nyuma na kuwaalika kwenye mahafali ya shule hiyo kama njia ya kuwahamasisha wanafunzi hao kusoma.

“Kuna wahitimu wenu wengi wanafanyakazi kwenye mashirika makubwa waleteni hapa ili wanafunzi waone kwamba hawako hapa kwa bahati mbaya wafanye vizuri kwenye masomo ili waje kuwa watu wakubwa,” alisema

Mkuu wa shule hiyo, Ntipoo Reca alisema mbali na kuwaandaa vizuri kitaaluma wahitimu hao, wamejitahidi kuwalea kwa maadili na anatarajia kuwa watakuwa watu wema wanakoenda.

“Tuliwapokea hapa mwaka 2020 tumewafundisha na wamekuwa wakifanya vizuri sana kwenye mitihani na tunatarajia kwenye mitihani yao ya mwisho watapata daraja la kwanza na daraja la pili,” alisema

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

ElimuHabari Mchanganyiko

Ugawaji taulo za kike watajwa kutokomeza utoro shuleni

Spread the loveBAADHI ya wanafunzi na walimu wa shule za sekondari mkoani...

ElimuHabari za Siasa

MbungeCCM ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the love  MBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze...

ElimuHabari za Siasa

Walimu 52,551 kupandishwa madaraja mwaka huu

Spread the loveNaibu Waziri wa nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala...

BiasharaElimu

NMB yatoa vifaa vya ujenzi kwa shule sita Nyasa  

Spread the loveBENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya ujenzi...

error: Content is protected !!