Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya NMB yatoa vifaa vya kuezekea kwa zahanati ya polisi Mtwara
Afya

NMB yatoa vifaa vya kuezekea kwa zahanati ya polisi Mtwara

Spread the love

BENKI ya NMB Kanda ya kusini imetoa vifaa vya kuezekea katika zahanati ya polisi iliyopo mkoani hapa vyenye thamani ya Sh17 milioni. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)

Vifaa hivyo ambavyo vitamalizia jengo la mama na mtoto katika zahanati hiyo ni pamoja na bati, mbao, misumari na mabati na kofia za bati.

Meneja wa benki ya NMB Kanda ya Kusini, Faraja Raphael Ngingo alisema kuwa changamoto za sekta ya afya nchini ni jambo la msingi kwa benki ya NMB.

Alisema pamoja na makubwa na mengi yanayofanywa na serikali katika sekta ya afya lakini NMB kama wadau wanao wajibu wa kuunga mkono juhudi hizo.

Meneja wa NMB Kanda ya Kusini – Faraja Ng’Ingo akikabidhi vifaa vya ujenzi kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Mwanahamisi Munkunda aliyeambatana na Kamanda wa Polisi Kikosi cha Afya Tanzania – ACP Dk. Hussein Yahaya na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara – ACP Nicodemus Katembo

“Tulipopata maombi haya ya kuchangia sekta ya afya tulifarijika na kuamua mara moja vifaa hivi ni moja ya ushiriki wetu katika maendeleo ya jamii, tunao wajibu wa kuhakikisha jamii inayotuzunguka inafaidika na faida tunayoipata” alisema Faraja.

Alisema wanatambua kuwa kupitia jamii ndipo wateja wanapotoka. Hata hivyo alisema NMB imekuwa ikipokea maombi mengi sana lakini imejikita katika afya, elimu na misaada ya majanga. Kwa miaka saba mfululizo sasa NMB imekuwa ikitoa asilimia moja ya faida yake kwa jamii.

Mganga mkuu wa zahanati ya polisi, ambaye pia ni mkuu wa kikosi cha afya mkoani Mtwara, Dk. Stephen Kisaka alisema zahanati hiyo ni moja kati ya vituo 18 vya kutolea huduma za afya mkoani Mtwara na ni moja kati ya vituo 37 vya jeshi la polisi.

Huduma zinazotolewa katika zahanati hiyo ni pamoja na wagonjwa wa nje, mama na mtoto na wenye maambukizi ya ukimwi na kwa mwezi huudumia wagonjwa 2500 mpaka 3000 na wenye bima ya afya 800 hadi 1000

Vile vile wanahudumia wagonjwa wa msahama, wazee na watoto wenye umri chini ya miaka mitano.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mtwara, Nicodemus Katembo alisema kuwa kituo hiko ambacho wagonjwa wanaohudumiwa asilimia 80 ni raia kilianza kwa wazo kutoka kwa askari polisi wenyewe na baadaye wakapata msaada kutoka kwa wadau.

“Tunataka ifikapo mwaka 2025 tuwe na kituo kamili cha afya kwa hiyo msaada huu utarahisisha njia ya kufika katika kituo cha afya kabla ya kufika mwaka 2025” alisema RPC Katembo.

Mmoja wa wagonjwa aliyefika hospitalini hapo kupata huduma, Rachel Thobias, alisema wanaishukuru zahanati ya polisi kwani huduma wanapokelewa na kuwapatia huduma nzuri kwa upande wa mama wajawazito, watoto na hata wagonjwa wan je.

Mkuu wa wilaya ya Mtwara, Mwanahamisi Mukunda alilipongeza jeshi la polisi kwa kuwa karibu na jeshi la polisi.

“Kama asilimia themanini ya wagonjwa wanaokuja hapa ni raia maana yake mko karibu nao na mnatoa huduma bora” alisema Mkuu wa wilaya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

error: Content is protected !!