Friday , 3 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Siku 100 za Silaa, atangaza mageuzi ardhi, atumbua vigogo
Habari za SiasaTangulizi

Siku 100 za Silaa, atangaza mageuzi ardhi, atumbua vigogo

Spread the love

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Jerry Silaa amesema Wizara yake inakusudia kufanya mageuzi makubwa ya kimfumo wa utendaji katika Sekta ya Ardhi nchini kwa lengo la kuboresha utendaji kazi katika utoaji huduma za sekta ya ardhi nchini.

Pia waziri huyo amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Anthony Sanga kuandika barua ya kumsimamisha kazi Mkurugenzi wa Maendeleo ya Makazi, Deogratius Kalimenze kwa kuendelea kutumia kanuni za viwango vya nafasi pamoja na za matumizi ya ardhi za mwaka 2018 ambazo aliagiza zisitishwe kutumika. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Matumizi ya kanuni hizo yametajwa kusababisha ongezeko la vituo vya mafuta, ukubwa wa mashamba ya mijini na mambo
mengine yanayoleta kero kwa wananchi.

Waziri Silaa amesema hayo leo tarehe 22 Desemba 2023 jijini Dar es salaam wakati wa kikao chake na Wahariri wa vyombo vya Habari kupitia Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kuhusu siku 100 tangu alipoingia kuhudumo ofisi hiyo alipoteuliwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Amesema wizara inakusudia kufanya mageuzi makubwa ya kimfumo wa utendaji katika Sekta ya Ardhi nchini ambayo yanalenga kuboresha utendaji kazi katika utoaji huduma za sekta ya ardhi.

Miongoni mwa maboresho hayo ni Programu ya Kupanga, Kupima, Kumilikisha ardhi (KKK) kwa kushirikisha sekta binafsi na mamlaka za upangaji ambapo katika maboresho hayo yatafanyika marekebisho ya utaratibu wa kukopesha fedha kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Viwanja utakaokuwa unatunza fedha na kukopesha fedha kwa ajili ya programu hiyo.

Aidha, amesema Wizara inakamilisha maboresho ya mfumo wa TEHAMA ambao utaruhusu huduma na miamala ya sekta kuanza kutolewa kidigitali na mfumo huo utaanza kutumika hivi karibuni kwa kuanza na mikoa ya Arusha, Tanga, Mwanza na Mbeya.

Ili kuendana na sayansi na teknolojia, Waziri Silaa amesema kuwa, Wizara hiyo imezindua rasmi mfumo wa ARDHI KLINIKI KIGANJANI maalumu kwa kupokea na kushughulikia malalamiko yatakayowasilishwa kwa kutumia simu ya kiganjani au kompyuta ili kuwahudumia watanzania kwa urahisi katika sekta ya ardhi.

Zaidi ya hayo Waziri Silaa amesema kuwa, Wizara ya Ardhi inafanya mabadiliko ya kimuundo na ya kiutendaji kwa kuanzisha mikoa maalumu ya ardhi katika maeneo yenye uhitaji mkubwa na kwa kuanzia imeanza na Mkoa wa Dodoma na Dar es Salaam.
Hata hivyo, amesema maboresho hayo yanaweza kuendelea kufanyika katika mikoa yenye miamala mingi ya ardhi ikiwemo Mkoa wa Mwanza na Pwani

Ameongeza kuwa, Wizara itadhibiti ujenzi holela wa viwanda na kuelekeza viwanda kujengwa katika maeneo ya kongani za Viwanda yenye huduma zote muhimu kama vile umeme, maji sambamba na kuongeza maeneo ya kutosha kwa ajili ya Kongani za Viwanda na kutolea mfano wa Kongani za Mlandizi, Kwala Chalinze na ile ya SinoTan Kibaha.

Akimkaribisha Waziri Silaa katika mkutano na Waahariri wa Vyombo vya Habari, Naibu Waziri wa Ardhi, Geophrey Pinda amesema kuwa, katika siku 100 za uongozi wake, Waziri mwenye dhamana ya ardhi ametoa dira na mwelekeo ili wizara iwe na matokeo mazuri ya kuwahudumia watanzania.

Kwa upande wake Kaimu Mwenyekiti wa TEF Nevile Meena ameshauri Serikali ijihusishe na mipango miji katika maeneo yote nchini badala ya kujihusisha na maeneo ya mijini tu kwa kuwa, kwa sasa miji mingi mipya inayofuata barabara imekuwa donda ndugu kwa kuwa haina mipango rasmi na kila mtu anajenga kiholela ikiwemo miji ya Kibaha, Picha ya Ndege, Kibaigwa na maeneo mengine nchini.

1 Comment

  • Silaa, umeanza vizuri, lakini maliza migogoro ya ardhi iliyoko kwenye vichaka vya Mahakama ya Ardhi. …miaka 30, 20, 10 anzia huko!
    Watu wa ardhi kama wataalamu waende…acheni kubabaisha!
    Wenzetu wanafanya hivi:
    1) Watu wa mazingira wanatenga maeneo ya mafuriko, yasiyokuwa salama na ya kulinda ndege na wanyama kiekolojia.
    2) Ardhi ya miundombinu ya maji safi, maji taka, umeme, gesi na kebo za optic zinapangwa na kuwekwa….siyo kusubiri au kubabaisha.
    3) Ardhi za viwanja vya makazi, maeneo ya maduka, soko, shule, park za kutembea, zimamoto n.k. yanapimwa kwa kuwianishwa na idadi za nyumba…wenzetu, kila nyumba 5,000 kuna park ya kutembea, bembea, n.k. kwetu, viliibwa na kujenga majumba.
    4) Maafisa ardhi wanafikishwa mahakamani kwenye migogoro inayohusu ardhi na kutoa utatuzi wa mgogoro, siyo Mahakama ya Ardhi isiyokutana haraka.
    5) Kama ardhi kapewa Asha, vipi Juma anadai ni yake?
    Wenzetu wanamlinda aliyepewa kwanza, akija mwongo na namba zake wanamshitaki.
    Dhuluma za matajiri dhidi ya maskini hazipo. Kwetu, Mfano, Dewji anataka kumdhulumu mjane ardhi, mnakaa kimya. Tumieni kikosikazi cha wanafunzi wa Ardhi wawaanike waovu. Magazeti nayo yachapishe bila yeye kutishia kutumia mahakama kwa sababu ana pesa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chadema waendelea kulilia katiba mpya

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeendelea kudai upatikanaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Kwahani

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi, imetangaza uchaguzi mdogo...

AfyaHabari za Siasa

Dk. Biteko aagiza utoaji huduma saratani usiwe wa kibaguzi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!