March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Shirika la Jhpiego lajipanga kupunguza vifo mama na mtoto

Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto

Spread the love

SHIRIKA la Jhpiego kupitia mradi wa Maternal and Child Survival Program (MCSP), linatarajia kupunguza vifo vya mama na mtoto nchini kutokana na idadi kubwa ya wanawake na watoto wanaofariki dunia kwa kasi, anaandika Moses Mseti.

Takwimu zinaonyesha kuwa wanawake 24 na watoto 144 wanaozaliwa hufariki dunia kila siku nchini na kwamba kila siku watu 168 hufariki kila siku.

Idadi hiyo ya wanawake na watoto wanaofariki dunia kwa siku ni sawa na watu 5, 040 kwa mwezi na 60, 480 kwa mwaka hatua ambayo inatishia kizazi kipya na ukuaji wa raslimali watu nchini.

Kauli hiyo imetolewa leo na Ndementria Vermand Mkurugenzi Msaidizi , Idara ya Mafunzo ya Uuguzi, wakati wa kuzitambua na kuzitunuku vyeti na ngao za utambuzi shule tatu za utabibu na ukunga ambazo ni Murgwanza, Kisare na Shirati kwa utoaji huduma bora.

Vermand amesema hali ya vifo nchini bado ni tishio kubwa ukilinganisha na nchi nyingine duniani ambazo idadi ya vifo vya mama na mtoto ni ya kuridhisha huku akidai wadau bado wanaendelea kufanya kupambana ili kupunguza vifo hivyo.

Mkurugenzi wa mradi wa MCSP, John George amesema lengo la mradi huo ni kuisaidia Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia na watoto kuboresha huduma ya ukunga na uuguzi nchini hatua ambayo italeta mabadiliko chanya ya akina mama na watoto.

“Tunafanya hivyo kutokana na mkoa wa Mara na Kagera kuwa na viwango vikubwa vya vifo vya mama na mtoto vinavyotokana uzazi na tumelazimikia kuteuwa vyuo 10 kutoka mikoa hiyo kusaidia kutoa Huduma,” amesema George.

George ameongeza kuwa wameshirikiana na wizara ili kuvijenga vyuo viweze kuboresha ujuzi wa wakunga na wauguzi wanaotoka kwenye vyuo hivyo huku akisisitiza ni jambo la muhimu kuwa na wataalamu katika sekta ya Afya.

error: Content is protected !!