March 6, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kesi ya Kubenea yazidi kupigwa kalenda

Saed Kubenea, Mbunge wa Ubungo

Spread the love

HATMA ya kesi ya mbunge wa Ubunge, Saed Kubenea (Chadema) inatarajiwa kujulikana kesho, anaandika Dany Tibason.

Kesho Mahakama ya Wilaya ya Dodoma itaamua ama itaendelea kuipiga kalenda kesi hiyo, kufutwa ama kusikilizwa.

Kwa mujibu wa Hakimu wa mahakama hiyo, James Karayemaha kesi hiyo itatajwa kesho baada ya leo Wakili wa serikali, Lina Magoma, kueleza kuwa kuna mambo mbalimbali ambayo yana mapungufu katika jarada la kesi ambayo inamkabili mbunge huyo.

Kubenea anashtakiwa kwa kosa la jinai ambalo anadaiwa kumshambulia mbunge wa viti maalum (CCM), Juliana Shonza wakati wa bunge la bajeti.

Hakimu James Karayemaha alipanga tarehe hiyo na wakili wa serikali, Lina Magoma, alikubaliana naye hivyo kesi hiyo itaendelea Septemba 5, mwaka huu.

Awali Kubenea alisema utaratibu wa kisheria uliotumika siyo mzuri hivyo ni vyema kesi hiyo ingebaki polisi hadi hapo upepelezi utakapokamilika na kwamba ni matumizi mabaya ya raslmali za serikali.

error: Content is protected !!