Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Sheria ya kupinga mapenzi jinsia moja yaanza kung’ata Uganda
Kimataifa

Sheria ya kupinga mapenzi jinsia moja yaanza kung’ata Uganda

Spread the love

POLISI katika wilaya ya Buikwe nchini Uganda inawashikilia watu wanne katika kituo cha polisi Njeru kwa tuhuma za kujihusisha na mapenzi ya jinsia moja ikiwa ni baada ya miezi mitatu ya utekelezaji wa sheria ya kupinga vitendo hivyo nchini humo. Anaripoti Isaya Temu, TUDARCo…(endelea).

Tarehe 19 Agosti 2023 Polisi wa kituo cha Njeru nchini Uganda kiliwakamata watu wanne wakiwemo wanawake wawili na wanaume wawili wanaotuhumiwa kushiriki mapenzi ya jinsia moja wakifanya shughuli hizo katika nyumba inayotoa huduma za kuchua na kukanda (maasage).

Msemaji wa polisi nchini humo, Fred Enanga aliwataja washukiwa hao kuwa ni Patricia Nantume, Hope Nawasasira, 20, Douglas Kibirige, 25, na Denis Kirumira, 27 ambao kwa sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Njeru.

“Eneo la tukio lilikaguliwa na upekuzi ulifanyika na vielelezo kadhaa vilipatikana, ikiwa ni pamoja na uume wa bandia, pakiti mbili za ladha ya shisha, chupa za mafuta yanayotumika kufanyia massage kama vilainishi vya ngono huku na tripod nne ambazo zimekuwa zikitumia kuweka kamera ili kunasa shughuli zao ambazo wanazichapisha kwenye TikTok,” alieleza Enanga.

Polisi katika wilaya hiyo imesema kuwa ilipata taarifa za siri kuwa wafanyakazi wanaofanya kazi ya kutoa huduma ya massage katika ofisi ya Cloud 9 massage and Chill outs ndipo ilifanyia kazi na kuwakamata watuhumiwa hao.

Hatua hiyo inakuja baada ya Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kutia saini kuwa sheria muswada wenye utata dhidi ya ushoga ambao unatoa adhabu kali dhidi ya vitendo hivyo.

Hata hivyo, Sheria hiyo inayotajwa kuwa mbaya na watetezi wa haki za binadamu, imezua taharuki na hasira kutoka katika mashirika mbalimbali ya kimataifa kama Umoja wa Mataifa, Benki ya Dunia pamoja na mashirika ya kutetea haki za binadamu huku nchi mbalimbali zilizokuwa zikiipatia Uganda misaada na mikopo, zikitishia kutohifadhili tena nchi hiyo.

Sheria hiyo pia imepata uungwaji mkono na Waganda wengi huku wabunge wakisema hatua hiyo ni muhimu dhidi ya madai ya ukosefu wa maadili katika nchi za Magharibi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

error: Content is protected !!