Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Njama za kuvuruga mkutano KKKT zafichuka
Habari za SiasaTangulizi

Njama za kuvuruga mkutano KKKT zafichuka

Mkuu wa KKKT, Dk. Fredrick Shoo
Spread the love

KUNA njama zinasukwa za kutaka kuvuruga mkutano mkuu wa Kanisa Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), kupitia kinachoitwa, “Kanisa Moja, Katiba Moja.” Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Taarifa kutoka Arusha zinasema, baadhi ya viongozi wanalazimisha kuwapo mabadiliko ya Katiba yanayolenga kuifanya KKKT kuwa na katiba moja, hoja ambayo inapingwa na wajumbe waliowengi.

Mpango wa Kanisa Moja, Katiba Moja, unadaiwa unalenga kumbeba Dk. Shoo, ili aweze kuendelea kuwa kiongozi wa kanisa hilo.

“Kuna watu wanataka kuvuruga mkutano wetu kwa kulazimisha Kanisa hili kuwa na Katiba moja. Nakuambia hivi, hatukubali. Hii ajenda ililetwa Shinyanga mwezi uliyopita, tukaikataa. Hatuwezi kuipitisha sasa,” ameeleza mjumbe mmoja wa mkutano mkuu wa KKKT unaofanyika jijini Arusha.

Anaongeza, “tunajua nani yuko nyuma ya mpango huu. Tunajua ni kipi kinacholengwa. Tunajua. Ni bora mkutano kuvurugika, kuliko kupitisha jambo hili.”

Mwandishi ameshindwa kumpata Askofu Shoo, kuzungumzia kadhia hiyo. Anaendelea kumtafuta.

Mara kadhaa katika maadhimisho ya miaka 60 ya KKKT, Askofu Dk. Shoo aliwalaumu wanaopinga mpango huo mbele ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!